NA FAUZIA MUSSA

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kuzifariji familia 98 zilizoathiriwa na upepo mkali uliovuma katika kijiji cha Tumbatu siku za karibuni.

Kufuatia tukio hilo lililotokea mwishoni mwa mwezi wa Agosti, Taasisi ya Sister Island imekabidhi kilo 1350 za mchele kwa wananchi hao.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi chakula hicho, huko Kichanagani katika Ofisi ya Wilaya ndogo Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Idrisa Kitwana Mustwafa, Alisema Serikali kwa ujumla imeguswa na tukio hilo, hivyo itaendelea kushirikiana na wadau ili kuhakikisha hali za wanakijiji hao zinarudi kama zilivyokuwa awali.

Aidha aliwataka wananchi hao kuwa wastahmilivu wakati serekali ikiendelea kuchukua hatua za kuwafariji kutokana na maafa hayo.

Kaimu huyo ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi alisema Serikali inayoongozwa na Dk. Hussein Ali Mwinyi iko pamoja na wananchi wake ikiwemo wa kijiji cha Tumbatu kwa hali zote na hivyo ujio wa Mkuu huyo katika kisiwa hicho ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar kuja kuwafariji wananchi wake.

Sambamba na hayo Mkuu huyo aliishukuru tasisi ya Sister Island kwa kushirikiana na Serikali kuwafariji wananchi wake kutokana na maafa hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Sister Island Haji Moh’d Ali alisema kama sehemu ya jamii tasisi hiyo imeamua kuzifariji familia hizo kutokana kuguswa na tukio hilo .

Alifahamisha kuwa Taasisi hiyo itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za jamii, na kuwashukuru wananchi na viongozi wa Mkoa huo kwa kupokea msaada huo na kuahidi kuendelea kuwa karibu na wananchi wakati wote.

Baadhi ya waathirika waliopatiwa msada huo akiwemo Kombo Mwadin Khamis na Miza Juma Haji walisema wanafarijika kuona wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali wapo karibu nao tangu yaliopotokea maafa hayo hadi kufikia sasa.

Itakumbukwa kuwa Agosti 22, 2024, upepo mkali ulivuma katika kisiwa cha Tumbatu na kuathiri mkaazi ya watu, nyumba za ibada na baadhi ya vipando katika mashamba ya wakulima wa kijiji hicho.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrisa Kitwana Mustwafa, akimkabidhi kipolo cha mchele mmoja wa wanachi wa Tumbatu aliepatwa na maafa ya upepo uliovuma katika kisiwa hicho siku za karibuni. (PICHA NA MPIGA PICHA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...