BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa mafunzo kwa wataalam kutoka vyuo na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha viwango vipya vya mabadiliko ya mtaala vinafuatwa katika utungaji wa mitihani, usahihishaji na uhakiki.
Akizungumza na wandishi wa habari Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu na Mafunzo wa NBAA, Peter Lyimo amesema kuwa wataalam wanaoshiriki mafunzo haya wana jukumu kubwa la kuandaa mitihani inayolenga kuwapa wahitimu wa CPA ujuzi wa kutosha kwa ajili ya soko la ajira.
"Mafunzo hayo yanahusisha utungaji wa mitihani, usahihishaji, na uhakiki wa mitihani ili kuhakikisha viwango vipya vya mabadiliko ya mtaala vinafuatwa ili kuleta tija kwenye soko la ajira katika kuwajenga wahasibu na wakaguzi wenye ujuzi na weledi sahihi". amesema Lyimo
Pia, wasahihishaji na wakaguzi wa mitihani wanapaswa kuzingatia malengo ya mitaala na matokeo ya ujifunzaji (learning outcomes), hasa tunapoingia kwenye masuala mapya ya sayansi na teknolojia kama vile sekta ya mafuta na gesi.
Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wamesisitiza umuhimu wa kujifunza mbinu bora za kuandaa na kusahihisha mitihani ili kusaidia maendeleo ya nchi kwa kuzingatia mabadiliko ya mitaala.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania ( NBAA) CPA Pius A. Maneno akifungua mafunzo kwa kwa njia ya mtandao kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali wanaotunga mitihani ya Bodi iliyofanyika katika Ofisi za NBAA jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu ya Taaluma na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo (kulia) akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali wanaotunga mitihani ya Bodi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...