WASHTAKIWA waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kumbaka na kumuingilia kinyume na maumbile binti wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma jana baada ya kuwatia hatiani kwenye mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Washtakiwa ambao kwenye video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii wakati wakifanya unyama huo wakidai wametumwa na afande walikuwa wanakabiliwa na kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Pamoja na hukumu Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya sh. milioni moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...