WAKULIMA wa zao la Pamba nchini wanatarajia kunufaika na zana za kilimo kufuatia ugawaji wa trekta 400, pikipiki 1000 na baiskeli 2500, boza 58 kwa ajili ya viuatilifu vya dawa na mbolea hai lita 3000.

Zana hizo zimekabidhiwa na Mhe. Hussein Bashe (Mb), Waziri wa Kilimo kufuatia ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Igunga, Mkoa wa Tabora tarehe 11 Septemba 2024.

“Serikali ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inalenga kuendelea kuwekeza kwa wakulima ili wazalishe mazao kwa tija. Na tutaendelea na mpango wa kuchimba mabwawa ili waanze pia kuvuna maji ya mvua na kuwa na Kilimo cha umwagiliaji,” amesema Mhe. Waziri Bashe.

Ameongeza kuwa ni vyema wakulima hao kutumia ipasavyo fursa na nyenzo hizo za kilimo na kupuuza baadhi ya wanasiasa.

“Serikali hii haiwezi kutoa dawa feki, mbegu feki na wanunuzi feki kwa wakulima. Siasa zinaleta uchochezi kwa wakulima zinaharibu maisha ya watu na hilo sitoruhusu huo mchezo kwenye Sekta ninayosimamia,” amesema Waziri Bashe.

Amefafanua zaidi kuwa “hatuwezi kuwa na Taifa linatukana watu, linatukana Serikali tunakaa kimya. Watu walikuwa na mateso walikopwa, pamba zilidoda. Miaka miwili tumetoa ruzuku ya mbolea bure na tutaendelea kufanya hivyo na tutaendelea kununua mazao.” Pia ameeleza nia ya wizara kuweka kituo cha ununuzi wa nafaka Wilayani Igunga.

Aidha, Mhe. Waziri Bashe ametumia fursa hiyo kueleza mipango ya Serikali ya kujenga mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji ya kutosha Igunga kwa kuwa kitakwimu ni ya kwanza au ya pili, hivyo ni lazima kuwa na uzalishaji wa uhakika kwa kilimo cha umwagiliaji cha Pamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...