CHAMA cha Wakulima wa Umwagiliaji wa Ruvu (CHAURU) kilichopo katika Kata ya Vigwaza, Mkoani Pwani chahimizwa kuwa na uwazi kwa wakulima kuhusu shughuli zake ili kuondoa sintofahamu zozote zisizo na tija.

Ameelekeza hayo Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) wakati wa mkutano wa hadhara na wana-ushirika na wakulima wa kijiji cha Visezi, Kata ya Vigwaza mkoani Pwani tarehe 4 Oktoba 2024.

“Tunataka kujenga ushirika wenye nidhamu hivyo ni vizuri muwe mnakaa na washirika na wakulima ili kuwapatia taarifa ya yale mnayofanya kwa uwazi. Hii itasaidia wajue mapato na matumizi ya Chama chenu,” amesema Waziri Bashe kwa Viongozi wa CHAURU.

Kuhusu mgogoro wa shamba la NAFCO kati ya Serikali ya Kjiji na CHAURU, Waziri Bashe amesema “kwa kuwa Ushirika upo chini ya Wizara ya Kilimo, basi suala hilo litashughulikiwa na Wizara ambapo tutatuma wataalamu ili kwa pamoja na Mkoa, Wilaya,CHAURU na Mrajis wa Vyama vya Ushirikia kupatikane makubaliano ya kulimaliza.

“Wizara ya Kilimo italilinda shamba hilo kwa maslahi ya wakulima wadogo na itahakikisha muafaka unapatikana, ikiwemo utambuaji wa mipaka halali na miundombinu ya asili, utambuzi wa waliouziwa shamba na waliopo ndani ya vigingi vya mipaka. Baada ya hapo tutakuja kufanya usanifu na kutangaza tenda ili mkandarasi akipatikana ajenge skimu za umwagiliaji ili aanze kazi, kwa kuzingatia utengaji wa eneo la kunyweshea maji mifugo,” amesema Waziri Bashe.

Kwa nafasi nyingine, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeelekezwa kukutana na washirika na wakulima nje ya CHAURU ili kuwe na mikopo ya vikundi, mikopo binafsi kwa wakulima waaminifu huku Chama hicho kikiwa mdhamini (group or individual financing with guarantee scheme).

Nayo Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imeelekezwa kukutana na washirika na wakulima kutatua changamoto za mbolea ili misimu ya mazao ikianza kusiwe na kero zozote.

Waziri Bashe pia alipata nafasi ya kukagua kiwanda cha kuchakata na kuzalisha mpunga wa tani 30 kwa siku. “Nipongeze hatua hiyo ambapo Serikali itaona namna gani isaidie ili muanze kuuza mchele wenu kwenye soko,” amesema Waziri Bashe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...