NA WILLIUM PAUL, SAME.

WATU watano wamefariki Dunia na wengine hishirini kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuingia kwenye daraja.

Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni alisema usiku wa kuamkia leo majira ya saa tisa usiku gari aina ya Costa iliyokuwa imebeba Wanakwaya wakitokea jijini Dar es salaam kuelekea Machame ilipofika eneo la Kirinjiko wilayani Same liliacha njia na kusababisha vifo hivo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, uchunguzi wa awali unabainisha kuwa Dereva wa gari hilo alisinzia na kupelekea gari hilo kuanja njia na kuingia kwenye daraja.

Alisema kuwa, kwa sasa majeruhi wanatibiwa katika hospitali ya wilaya ya Same.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...