.jpg)
JESHI la Polisi limesema hakuna tukio kama ambalo limetokea au kuripotiwa eneo lolote nchini kwetu.
Katika taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David A. Misime – DCP
imeeleza kuwa Kuna picha mjongeo (video clip) isiyokuwa na sauti inasambaa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye makundi binafsi kama inavyoonekana kushoto mwa taarifa hii.
"Tunaendelea kufuatilia kwanini aliyeanza kuisambaza ametoa sauti."
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa, Jeshi la Polisi wanayo mashirikiano ya kikanda na Majeshi mengine ya Polisi tutawashirikisha ili kupata chanzo cha picha hiyo mjongeo ni ni nini, ni tukio gani na limetokea wapi.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa wito kwa wanaoendelea kuisambaza au aliyenayo wasiendelee kuisambaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...