Na Linda Akyoo - Moshi.
Baada ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri jeshi Mkuu Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Majeshi,Jenerali Jacob John Mkunda, na kumpa jukumu la kupandisha Mwenge huo kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro kazi hiyo ilitekelezwa mara moja.
Kikosi kilichokabidhiwa Mwenge wa Uhuru kina jumla ya Wanajeshi 21,na Leo tarehe 15 Oktoba,2024 wameanza safari ya kuelekea katika kilele cha mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe.Nurdin Babu ameshindwa kujizuia na kueleza namna alivyo farijika na ujio wa Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Kilimanjaro kwa mara ya pili ndani ya mwaka 2024, na kusema kuwa tumefarijika sana kwani Mwenge umerudi nyumbani.
Mhe.Babu ameyasema hayo leo tarehe 15 Oktoba, 2024 wakati wa kuupokea Mwenge wa uhuru katika geti la mlima Kilimanjaro lililopo Marangu mkoani Kilimanjaro na kumshukuru Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuurudisha mwenge huo Mkoani hapo.
Aidha RC Babu amewakumbusha wana Kilimanjaro kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru "Tunza Mazingira,Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu" na kutoa rai kwa wananchi kujiandikisha ili kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.
Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda ameahidi kuwa watatekeleza jukumu walilopewa la kufikisha Mwenge wa Uhuru pamoja na Bendera ya Taifa katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...