Na Linda Akyoo -Moshi

Historia nyingine imeandikwa Leo tarehe 15 Oktoba,2024 mara baada ya kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania kuanza safari ya kupandisha Mwenge wa Uhuru pamoja na Bendera ya Taifa mpaka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa kuwaaga Wanajeshi hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Jakaya Kikwete amesema kuwa kikosi kwa mara ya kwanza Mwenge wa Uhuru uliwashwa na Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961,akitekeleza kwa vitendo maneno yake ya kifalsafa aliyoyatamka katika Baraza la Kikoloni

Aidha Mhe.Kikwete ameeleza dhamira ya Mhe Raisi kupeleka Mwenge wa Uhuru katika kilele cha mlima Kilimanjaro inatokana na mbio zenyewe kutimiza miaka 60 tangu zianze kuasisiwa mwaka 1964,muungao wa Tanganyika na Zanzibar na mapinduzi matukufu ya Zanzibar pamoja na miaka 25 tangu Baba wa Taifa atutoke na Tanzania imeendelea kuishi katika maono yake.

Sambamba na hilo Mhe.Kikwete amesema kuwa Leo tunapeleka Mwenge wa Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro ili kutangazia Dunia kuwa Muungano wetu ni imara na tumeendelea kuyalinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwa kutumia falsafa ya Mwenge wa Uhuru na Mlima Kilimanjaro.

Kwa upande wake Waziri wa Vijana,Utamaduni na Michezo kutoka Zanzibar Fatma Hamad Rajab amesema kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unatuunganisha na Mhe Raisi amefanya mengi katika kuhakikisha Muungano wetu unakuwa imara na kumshukuru Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe Nurdin Babu kwa napokezi mazuri.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...