WAZAZI wameswa kuzingatia mlo kamili kwa watoto, jambo litakalo wasaidia watoto hao kuwa na afya bora na uwezo wa kumudu masomo vyema.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe Duniani, katika Kata ya Jangwani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo,Diwani wa kata hiyo, Zacharia Digos, alisema ni siku muhimu kwa wazazi na watoto hususan wanafunzi.

Alisema, elimu inayotolewa kuhusu afya na lishe kamili inaumuhimu kwa jamii hasa watoto ambao kwani husaidia kukua vizuri, kuwa na afya njema na kuwa na ufahamu mzuri wawapo darasani.

“Tunawapa elimu ya afya na lishe bora watoto ili wajue mlo kamili na wakawe mabalozi wetu kwa wazazi wakirudi nyumbani,”alisema Diwani Digos.

Alieleza, wazazi na walezi wanapoandaa chakula ni muhimu kuzungatia mlo kamili kwa mtiririko mzuri jambo linalosadia watoto kukua kwa afya.

Awali Ofisa Mteji Kata ya Jangwani, Ally Mkumbukwa, alisema maadhimisho hayo ni ya Dunia lakini yamefanyika kwa ngazi ya kata.

“Katika ngazi ya kata tuliona ni vyeka tusherehekee katika Shule ya Msingi Mnazi mmoja.Elimu muhimu ya afya na lishe imetolewa. Lengo wanafunzi waipeleke kwa wazazi wakawe mabalozi wetu,”alisema Mkumbukwa.

Ofisa Lishe wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Neema Mwakasege, alisema wazingatie makundi sita ys chakula wanapo andaa mlo.

Alisema mlo hui uhusishe chakula cha nafaka, mizizi, matunda, mbogamboga, mafuta na protini.

“Hivyo katika maadhimisho haya tumepata fursa ya kuwafundisha wanafunzi kuhusu mlo kamili ambao unapatikana katika makundi hayo mbalimbali ya chakula,”alisema Neema.

Alieleza katika maadhimisho hayo walipima ukuaji wa watoto ambapo asilimia kubwa walibainika kuwa na afya bora huku wachache wakibainika kuwa na utapiamlo wa hatua za awali.

“Tuliwabaini kuwa na changamoto tukewasiliana na walimu waongee na wazazi husu namna bora ya kutatua changamoto hiyo,””

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mnazi mmoja, Karuki Nacho, alisema shule hiyo imekuw ikitoa chakula kwa wanafunzi hivyo kuhimizs walezi, wazazi na wadau kuzingatia wanachangia.

“Nashukuru kuna mwamko mkubwa wa wazazi kuchangia kwani mtoto akipata chakula shuleni inasaidia kumjenga kiafya na kiakili darasani,”aliisema.

Wanafunzi wa Shule hiyo wameishukuru Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Kwa kuanzisha utaratibu wa kuwapatua chakula shuleni uliowafanya kuwaongezea bidii na uelewa darasani hivyo kuongeza ufaulu.

Maadhimisho hayo hufanyika kwa zamu katika kata zote za Jiji la Dar es Salaam na handaliwa na Ofisi za Maofisa Watendaji wa Kata .




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...