Na Oscar Assenga, Pangani

Waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza mkandarasi anajenga mradi wa maji wa miji 28 kuhakikisha unakamilika kabla ya wakati Ili kuwaondolea wananchi adha ya ukosefu wa maji.

Maagizo hayo ameyatoa wilayani Pangani wakati alipotembelea ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji katika eneo la Madanga na kimang'a

" Huu mradi fedha zake zipo tayari hivyo nimtake mkandarasi aongeze nguvu kazi Ili uweze kukamilika kabla ya wakati wake na wananchi waweze kupata huduma karibu na maeneo yao"amesema Waziri Aweso.

Mradi wa maji wa miji 28 unatekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Tanga ambapo msimamizi wa mradi huo Mhandisi Yohana Mgaza amesema kuwa mradi huo mpaka Sasa umefikia asilimia 60.


"Mradi unatarajiwa kujenga matanki ya kuhifadhi maji nane na tayari bomba zimeshalazwa umbali wa zaidi ya km 107 kati ya 188 yanayohitajika"amesema Mgaza.


Mradi wa maji wa miji 28 ulitikiwa ukamilike mnamo mwezi Disemba mwaka 2025 hata hivyo unatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwakani huku ukiwa tayari umefikia asilimia 60





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...