Na Oscar Assenga, Kilindi 

Waziri wa maji Jumaa Aweso ametoa siku 60 Kwa  mameneja wa maji wa Mamlaka ya mji mdogo songe na RUWASA wilaya Kilindi kubadilika kiutendaji kuleta matokeo chanya ya changamoto ya huduma ya maji kwenye wilaya hiyo 

Hatua ya kauli ya Waziri huyo inatokana na kutokuridhishwa na utendaji wao hasa katika kuhakikisha wanawapatia wananchi maji huduma ya maji  safi na salama katika mji wa Songe na Bokwa 
Aliyasema hayo  wakati akizungumza na wataalamu wa Ruwasa wilaya ya Kilindi na Mamlaka ya  Mji Mdogo Songe ambapo alisema kwamba lazima viongozi hao wabadilike waonyeshe dhamira ya dhati ya kuwasaidia wananchi wa mji huo kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo yao.

Vile vile alimpaka siku 60  Mkurungenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule kufanya utafiti wa vyanzo vya maji ya ardhi katika eneo la Bokwa na kusimamia uchimbaji wa visima kuhakikisha kazi hiyo ianze ya kufanya tafiti ya uhakika kuhakikisha wananchi wanapata maji ya uhakika katika eneo la Bokwa na Songe .

"Niwaambie kwamba nyie ni wataalamu wa Maji hapa Kilindi tufanye kazi kwa waledi kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji na kama mtafanya vile kawaida nitawaondoa  hivyo badilikeni na faraja ya mradi wa maji ni watu wapate maji"Alisema 
Aidha aliwataka wafanye tafiti na waisimamie na wajue kwamba lita walizozikadiria wanakwenda Ili kuwasaidia wananchi wa mji wa Kilindi na maeneo mengine kupata huduma ya uhakika ya maji na kuondokana na adha waliokuwa wakikumbana hayo awali.
Awali Mbunge wa Jimbo la Kilindi Omari Kigua aliiomba serikali kuhakikisha utekelezaji wa mradi wa maji Kwediguluma ambao utaweza kuwa suluhu ya Kudumu ya changamoto ya maji kwenye wilaya hiyo.
"Wilaya hii Ina vijiji 102 na vitongoji 613 lakini eneo kubwa halina huduma ya maji hivyo Kwa utekelezaji wa mradi huo utamaliza changamoto katika eneo kubwa la wilaya hiyo"alisema Kigua.
Awali Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji alisema kuwa kuna miradi mitano ambayo ipo katika hatua za ukamilikaji kinachohitajika ni fedha tuu Ili iweze kumalizika.

"Serikali ilituletea mradi wa sh Bil 22 lakini bado haujaanza hivyo tunaomba Waziri itusaidie kutilia mkazo Ili mradi huo uweze kuanza na kuweza kuleta matokeo chanya Kwa wilaya yetu katika changamoto ya uhaba wa maji"alisema DC huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...