Na Lilian Ekonga............
Shirika la Msichana Initiative na shirika la Norwegian Church Aid wamekutana na viongozi wa dini mbalimbali kutoka mikoa zaidi ya 10 kwa lengo la kujadili na kujenga uelewa kuhusu mabadiliko ya umri wa ndoa.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano huo Mkurugenzi wa Shirika la Msichana intiative Rebeka Gyumi amesema wamekutana na viongozi wa dini kuona mchango wao katika swala la umri wa chini wa kuoa na kuolewa na kuangalia kwa mapana yake uzoefu wa nchi mbalimbali kwenye maswala la mbadiliko ya umri wa ndoa.
Rebeka ameongeza kuwa wameona ni vyema kuwashirikisha viongozi wa dini kwa sababu wamekuwa na ushawishi mkubwa na wanauwezo wakuwa fikia kundi kubwa la watu na kulibeba hilo swala katika namna ya kuleta badiliko.
"Tunafahamu mchango wa viongozi wetu wa dini katika kuhakikisha hili kuweza kufanikiwa na wanaisaidia serikali kuweza kufikia lengo mahususi na tunajifunza kwamba tunapoendelea kuongea na viongozi wa dini ndo wanajifunza hili swala na kuona mchangio wao na nafasi na kuhakikisha tunatokomeza ndoa za utotoni" amesema Rebeka
Kwa upande Sara shija msimamizi wa Miradi ya Norwegian Church Aid Tanzania amesema mkutano huo ni muendelezo wa mijadala kuhusiana na ndoa za utotoni ambapo wamekuwa wakiongea na viongozi dini kwenye changamoto ya Ndoa za utotoni na ukatili wa kinjinsia
Amesema kuwa wamekuwa wakiongea na wadau vijijini kuhusiana na mila potofu kandamizi zinazoumiza jamii na wameona viongozi wa dini wanafasi katika kuleta mabadilko ya kisheria hasa kwenye eneo la umri wa mtoto wa kike kuolewa.
"Tuko kujadili na viongozi wa dini kutoa namna tunafikia lengo na sheria kumlinda mtoto wa kike kuepukana na changamoto ya kuolewa.chini ya miaka 18"amesema shija
Nae Rachael Boma kutoka kutoka shirika la UN woman amesema ni jambo muhimu la kuzungumza na viongozi wa dini kwa kufikiria umuhimu wa wanawake na wasichana katik nchi ya Tanzania.
"Kuna nchi mbalimbali ambazo zimefanya mabadiliko ya kisheria, na tunaomba kweny vitabu vya dini wanaweza kutafisiri hichi kitu kina dhalilisha wasichans" amesema Boma.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bakwata shekh Khamisi Lugome ameseama wao wanakubaliana na umuhimu wa kutenda uhadilifu wa kuwapa nafasi sawa mtoto wa kiume na wakike katika maswala mazima ya kupata elimu
"Watoto wakike wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo changamoto ya kuwazuia kutekeleza malengo hasa ya kielimu"amesema
Amesema katika mlinda mtoto wa kike iwekwe sheria ambayo itamlinda na mtoto wa kike mpaka atapo maliza elimu yake ya sekondari kidato cha nne mpka sita ndipo aweze kuolewa.
Mchungaji Monica Lugome kutoka kanisa la CCT amesema kumlea mtoto katika maadili mema ni kuhakikisha mtoto anapata haki zake katika nanja zote ya kupata Elimu, afya bora
"Sisi kama kanisa hatuungi mkono ndoa za utotoni kwa mtoto wa kike , nawasihi viongozi wenzangu wa dini tusimame kwenye maandiko bado tuna nguvu ya kumlinda mtoto wa kike kwenye ndoa za utotoni mpaka atapokuwa mtu mzima" amesema.
Padri Longino amesema kanisa haliungi mkono katika ndoa za utotoni maan ndoa inawajibu na misingi yake na wanamtaka mtu atakaye ingi kwenye ndo awe n Kili timamu kimwili, kiroho na ukomavu wa kiimani ya kikristo na kikatoliki
"Natoa wito kwa watu wanaozesha mabinti wadogo kwa maana wanapingana na mapenzi ya Mungu na uhalisia kwa kumlazimisha mtoto kuingia kwenye ndoa kwa kumpa majukumu makubwa ya kuwa mama"amesema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...