Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uongozaji Ndege katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bi Flora Alphonce amefungua Mkutano wa mwaka wa Watumishi wa Idara ya Huduma za Uongozaji Ndege kwa kuwakumbusha wajumbe wa Mkutano huo kwamba kikao hicho licha kukumbashana majukumu yao ya kazi lakini pia ni kikao cha mafunzo zaidi.
Kwenye kikao hicho ilitolewa Mada ya Afya ya Akili na Dkt Garvin Kweka kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa washiriki wa Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya TCAA, jijini Dar es Salaam, Novemba 28, 2024.
Katika mada yake Dkt Kweka aliwaasa Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wa Idara ya Huduma za Uongozaji Ndege kuwa makini na kuepuka tabia zinazoathiri utendaji kazi wao ili wasikupambane na changamoto mbalimbali wanapokuwa kazini na hata katika maisha yao binafsi.
Mada hiyo ya Dkt Kweka, ilijikita zaidi katika kutoa mafunzo kuhusu uelewa wa wafanyakazi kuhusiana na madhara ya uraibu na jinsi ya kuboresha ufanisi kazini.
Dkt. Kweka alisisitiza kuwa, uraibu unaweza kusababisha changamoto kubwa kazini na katika maisha binafsi ya wafanyakazi, hivyo ni muhimu kudhibiti mienendo inayoweza kupelekea matatizo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...