KATIKA kukuza ufanisi wa operesheni za kampuni ya Airtel katika soko la Tanzania na nchi zingine barani Afrika, imemchagua Charles Kamoto kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Airtel Tanzania kufuatia mabadiliko ya uongozi yaliyofanyika Afrika.

Katika taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel Africa Group, Sunil Taldar, imeeleza kuwa mabadiliko hayo ya uongozi ni mkakati unaoendana na matarajio ya Airtel Group katika kuongeza nafasi ya Airtel katika soko la Tanzania na kuchagiza maendeleo endelevu kama mtoa huduma za mawasiliano anaeongoza nchini.

Charles atachukua nafasi hiyo mpya kutoka kwa Dinesh Balsingh ambae ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Nigeria, kuanzia Novemba 1, 2024.

Awali, Dinesh alikuwa akitumikia nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania ambapo aliweza kuchangia mafanikio makubwa katika ukuaji wa soko la mapato ya hisa kupitia mbinu za kimkakati za masoko, ubunifu wa bidhaa na utekelezaji katika soko lenye ushindani wa hali ya juu tangu alipochukua wadhifa huo mwezi Februari 2022.

Charles Kamoto, ambae ana uzoefu wa miaka 24 katika sekta ya mawasiliano ikiwemo miaka 17 katika nafasi kubwa za uongozi – alijiunga Airtel Malawi kama Afisa Mkuu wa Biashara na baadae alianza kupanda ngazi za juu hadi kufikia nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji mwaka 2016.

Uongozi wake imekuwa na mchango mkubwa katika kufikia mafanikio ya faida, kuongeza wateja na soko la hisa ikiwemo uzinduzi wa Airtel Money Malawi kama chapa ya huduma jumuishi za kifedha inayoongoza. Mwaka 2020, Charles alichangia kuwekwa kwa Airtel Malawi katika soko la Hisa la Malawi, na kuongeza nguvu ya uwepo wa kampuni hiyo katika ukanda huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...