*Asema ni matukio yanayotokea kwa vyama vyote, sio wapinzani peke yao


* Aliomba Jeshi la Polisi kuchunguza na kukamata waliohusika

Na Mwandishi Wetu
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) CPA Amoss Makallla amesema Chama hicho kinalaani matukio mbalimbali yaliyotokea yakiwemo ya mauaji na watu kujeruhiwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Aidha amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi ili kubaini waliohusika ili Sheria ichukue mkono huku akieleza kuwa yanapotokea matukio ya mauaji na watu kujeruhiwa ni vyama yakazungumzwa kwa pande zote kwani wapo makada na viongozi wa CCM wamejeruhiwa na kuuawa.

CPA Makalla ameyasema hayo leo Novemba 29,2024 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akıtoa sababu ambazo zimekifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza matukio ya watu kushambuliwa na kuuliwa wakati wa kampani za uchaguzi wa Serikali za mitaa.

“Nataka niliweke wazi hili matukio haya yasihusishwe na vyama vya upinzani tu yaaani tusiongelee kwa kukemea jambo hili kwamba vyama vya upinzani vinawatu ambao wamepatwa na matukio haya halafu tukasahau kama Chama Cha Mapinduzi nacho kimefanyiwa matukio kama haya.

“Naomba niliweke tunapokemea tukemee wote kwa pamoja ,tunapoeleza kasoro ni kwa wote, Kwahiyo hawezi kutokea mtu akakaa na kisha anaandika statement yake kwamba kumetokea mauaji na ukaeleza kwa wafuasi wenu bali tulikemee kwa nchi nzima kwa maana mauaji,kujeruhiwa kwa watu,kupigwa ni kwa vyama vyote .Nipo hapa kwa vyama vyote lakini ninataka kuweka rekodi sahihi.

“CCM kwa taarifa tulizonazo na niwakumbushe kuna makada sita waliofanyiwa vitendo vya kupigwa,kujeruhiwa na kuuawa, ninyi ni mashahidi kwamba Novemba 13 mwaka huu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilolo Christina Bikibiki aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake na watu wasiojulikana,” amesema.

CPA Makalla amesema kwa hiyo isije mtu kauawa lakini wa Chama cha Mapinduzi hatajwi kwani matukio hayo yametokea na Chama hicho kinalaani huku akisisitiza Jeshi la Polisi limeendelea na uchunguzi lakini bado wanaamini kwanini litokee tukio wakati wa uchaguzi.

Akieleza zaidi amesema kuwa anayo taarifa ya makada wanne wa CCM wamejeruhiwa vibaya Rorya na Tarime wakati wa uchaguzi huu wa Serikali za mitaa lakini kuna kada mwingine Songwe katika Kijiji cha Nakawale mpaka sasa yuko mahututi baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali wakati wa uchaguzi

“Kwa hiyo tunaposema jambo hili isionekane tu kwa upinzani tukasahau na CCM pia wamefanyiwa jambo hili na niko hapa kukemea matukio yote yaliyofanyika kwa wote lakini kuwakimbusha wako makada na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wamepoteza maisha wameuawa kama ili toto kwa kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kilolo na makada wengine kujeruhiwa,amefafanua.

CPA Makalla amesema matukio hayo yote wameyarekodi na kusisitiza Chama chao kinakemeea mauaji na vurugu ambazo zinafanywa na baadhi ya watu wakati wa kampeni za uchaguzi.

Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi,Uenezi na Mafunzo CPA Amoss Makalla, Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Novemba 29, 2024

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...