Na Said Mwishehe,Michuzi TV
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makalla amesema Chama hicho kimepokea kwa mshutuko taariifa za kifo cha Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dar es Salaam Dk.Faustine Ndugulile na kwamba kifo chake ni pigo kwa Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla na atamkumbuka kwa jinsi alivyokuwa na upendo kwa wananchi wa Jimbo lake.
Akizungumza leo Novemba 27,2024 baada ya kushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijiji na Vitongoji ,CPA Makalla ametoa masikitiko yake kwanza akiwa kama Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi lakini kama Mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam na namna ambavyo amewahi kufanya naye kazi Dk.Ndugulilnimewahi alipokuwa Mbunge.
"Chama tumepokea msiba huu kwa masikitiko makubwa,tumeshtushwa kwasababu Dk.Ndugulile alikuwa anaiwakilisha Tanzania katika anga za Dunia kwani alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani(WHO)Kanda ya Afrika nafasi ambayo ameipata akiwa Mbunge wa Cha Mapinduzi .Dk.Ndugulile alikuwa kada mwaminifu ,mtu mwenye weledi,ametumikia nafasi mbalimbali ikiwemo ya Naibu Waziri na baadae Waziri.
"Kwahiyo Dk.Ndugulile alikuwa anaiuza nchi yetu katika anga la Dunia ,kwa hiyo ni pigo kubwa kwa Taifa na Dunia kwasababu alikuwa anaenda kuwa katika nafasi kubwa ya kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani,"amesema CPA Makalla na kuongeza Chama Cha Mapinduzi kinamlilia.
Akielezea zaidi CPA Makalla amesema yeye kama Mlezi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye anayalea majimbo yote ya na Wilaya za Mkoa huo anaelewa kazi ambazo alikuwa anazifanya Dk.Ndugulile."Nimefanya naye kazi nikiwa Mkuu wa Mkoa, ni mtu ambaye anapenda watu wake,anapenda kushughulika na matatizo ya watu wake na muda wote.
"Alikuwa ni mtu aliyekuwa anawapenda wananchi wake wa Kigamboni na ukweli wananchi wa Kigamboni wamepoteza kiongozi mzuri na mfuatiliaji. Tunamuombea kwa Mungu apate pumziko jema,"amesema CPA.Makalla.
Akizungumza kuhusu mchango wa Dk.Ndugulile Bungeni,.CPA Makalla amesema akiwa Mbunge alifanya naye kazi na ukweli alikuwa ni Mbunge anayejua kujenga hoja kuhusu mambo yake yanayohusu sekta mbalimbali na hasa sekta ya afya kwasababu alikuwa mtaalam na mbobevu wa sekta hiyo,hivyo Taifa limepoteza mtalaam.
Pamoja na hayo amesema Dk Ndugulile na enzi za uhai wake hakuwa mtu wa kukata tamaa na kuelezea hata safari yake ya Ubunge licha kwamba alikaaa sana Afrika Kusini lakini apofika Kigamboni alikuwa Mbunge na amekaa katika Jimbo hilo kwa muda mrefu akiwatumikia wananchi wake kwa upendo mkubwa.
Dk.Ndugulile amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Novemba 27,2024 nchini India na kwa sasa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...