Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu)Ridhiwani Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa ushirikishaji wa jamii katika utunzaji na ukarabati wa miundombinu ya barabara nchini.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua  mradi uitwao CBRM kwa ajili ya ushirikishaji wa jamii katika ukarabati wa miundombinu ya barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA).

Mradi huo ni sehemu ya mradi mkubwa uitwao RISE,  unatekelezwa na TARURA kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia.

Waziri Ridhiwani amesema kuanzishwa kwa Mradi wa Ujenzi na matengenezo ya barabara kwa kutumia Vikindi Vya kijamii(CBRM) unakwenda kuboresha hali za uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Amesema sekta ya kazi na usafirishaji zinachochea maendeleo y ukuaji wa uchumi nchini nyingi ikiwemo Tanzania kwa hiyo uwekezaji unaokwenda kufanyika katika maeneo hayo ni wazi utaongezeka Kasi ya ukuaji uchumi wa nchi pamoja na kubadilisha uchumi wa mtu mmoja mmoja katika maeneo yanayotekeleza mradi.

“Naamini mradi huu unakwenda kutatua baadhi ya kero katika Jamii hasa ambako Mradi wa CBRM unakwenda kutekelezwa kwani utasaidia kutatua changamoto kwa kuwajengea uwezo wananchi wanaojihusisha na mradi lakini unakwenda kuongeza ujuzi pamoja na kutengeneza watalaam.

Amesema katika utekaji wa miradi ya miundombinu ya barabara ushirikishwaji wa jamii  hasa vikundi vilivyo hatarini kupoteza matumaini ya kujikomboa katika uchumi yakiwemo vijana hususani wasiokuwa na ajira , wanawake na hasa wenye ulemavu ni muhimu yakapata fursa ya kujikomboa kiuchumi kupitia miradi ya aina hiyo.

Waziri Kikwete amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza bajeti ya maendeleo ya miundombinu tangu aingie madarakani. Kwamfano hadi kufika mwaka 2024  bajeti ya mwaka ya TARURA imeongezela mpaka kufika Sh.bilioni 850 kutoka Sh.bilioni 275 .

“Fedha hizo zilizoengezwa zinalenga kusaidia kuboresha maisha ya wananchi kupitia uboreshaji wa miundombinu na ujenzi wa   barabara na kupitia uwekezaji huu uliofanywa na Rais Samia mtandao wa barabara umeongezeka mpaka kufikia kilometa 3,337 za barabara kinyume ilivyokuwa imepangwa kufikia kilometa 3100 ifikapo  mwaka 2025.

“Sera ya Taifa ya usafiririshaji inasisitiza kuhudumiwa watu wenye mahitaji maalum hususani watu wenye ulemavu,watu wa Vijijini , vikundi vinavyotengeneza lakini na wakulima.Pia  kufungua fursa za kiuchumi pamoja na changamoto kubwa za uhamiaji.”

Akizungumza zaidi katika uzinduzi huo amesema pamoja na hayo anafahamu Shirika la Kazi Duniani(ILO)limekuwa likifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ,Wakala na idara mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa huduma bora kupitia miradi ya kuboresha maisha ya wananchi na kusisitiza  ILO imekuwa ikisaidia kujenga uwezo wa taasisi za umma na binafsi nchini.

“Wizara yetu inathamini juhudi za ILO katika kuimarisha  na kujenga uwezo wa TARURA  na taasisi nyingine na Wizara itaendelea kusimamia miradi ya aina hiyo kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi hasa katika eneo la ajira,”amesema
Waziri Kikwete.

Kwa upande wake Bi Caroline Khamati, ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) amesema kuwa lengo maalum la mradi huo wa CBRM  ni kuhakikisha kunakuwa na ushiriki  endelevu na ushiriki wa vikundi vya jamii hasa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu  na wengine ni watu waliohatarini katika matengenezo ya mara kwa mara ya Vijijini .

Ameongeza kwa kupitia  ujuzi na uzoefu wa Shirika la Kazi Duniani(ILO) katika eneo hilo ni matumaini yake kwamba malengo yaliyopangwa yatafikiwa huku akimpongeza Rais DK.Samia Suluhu Hassan kwa kuisaidia ILO kutekeleza majukumu yake  na kuahidi Shirika hilo litaendelea kushirikiana  na Tanzania kuboresha huduma.

“ ILO inafanya kazi zake kwa karibu zaidi kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania ,imefanya kazi katika maeneo mengi.ILO tunajivunia kuwa katika nchi ambayo  ni mwanachama wa Shirika la Kazi Duniani.”

Awali Mtendaji Mkuu wa TARURA, Injinia  Victor Seff amesema kwamba ushirikishwaji wa jamii katika utunzaji miundombinu ya barabara ni muhimu kwani pia inafanya umiliki wa miundombinu hiyo kuwa chini ya jamii.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...