WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), tarehe 25 Novemba 2024, ameshiriki Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Magu, kwa kuwanadi na kuwaombea kura Wagombea wa nafasi za Wenyeviti wa Vitongoji, Mitaa, pamoja na Wenyeviti wa Vijiji kupitia Chama hicho katika Kata za Kandawe, Nkungulu pamoja na Kata ya Ng’haya katika vijiji vya Ihimbili, Nhobola na Bugatu

Akiongea  katika  kuwanadi wagombea hao wa chama cha Mapinduzi,Dkt. Stergomena Tax, amewaomba  na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuwachagua Wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kiendelee kushika dola na kuwaletea maendeleo.

Akifafanua zaidi, Dkt. Tax amekumbusha kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya Chama cha Mapinduzi, kupitia kwa Mwenyekiti wake  Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika nyanja mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu,  Ujenzi wa vituo vya Afya, Ujenzi wa vyumba vya madarasa na Miradi mingine mikubwa ya Kimkakati ni uthibitisho tosha kwamba Chama cha Mapinduzi ndicho Chama pekee kinachoweza kuwaletea maendeleo Wananchi.

Hata hivyo, Dkt. Stergomena Tax amewakumbusha Wananchi wa Kata za Kandawe, Nkungulu pamoja na Ng’haya kutokuridhika na shamrashamra za Kampeni na Mikutano kufurika watu, bali kila mmoja anapaswa kuhakikisha anakwenda kupiga kura tarehe 27 Novemba 2024 na amewakumbusha kuwa, hakuna Mgombea atakayepita bila kupingwa bali kura nyingi za Mgombea ndizo zitakazompatia Ushindi wa mtaa, kitongoji, kijiji au kata.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...