NA FAUZIA MUSSA

Katika kuadhimisha miaka minne ya Dk. Mwinyi, shirikisho la kabadi Zanzibar limeandaa ligi ya mchezo huo msimu wa kwanza ambapo kufanyika kwa mashindano hayo kutasaidia kuutangaza mchezo huo ndani ya jamii.

Hayo yameelezwa na ofisa michezo kutoka idara ya michezo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Saleh Hashim wakati akizindua mashindano hayo yatakayodumu kwa siku tano katika viwanja vya New Amaani Compex.

Alisema uzowefu unaonesha kuwa mchezo huo bado ni mgeni kwa jamii hivyo aliwaomba vijana kujifunza kupitia mashindano hayo.

Alieleza kuwa Wizara inafarajika kuona michezo mbalimbali inaongezeka hali inayosaidia kuitangaza nchi na kusema kuwa wizara itaendelea kuchukua juhudi za makusudi kuhakikisha mchezo huo unatambulika na kuendelezwa.

Alifahamisha kuwa hatua hiyo pia inaonesha wazi maendeleo ya mchezo huo ulioanzishwa miaka miwili iliyopita, na kuwaomba wadau wa michezo kuongeza nguvu katika mchezo huo ili kuupa thamani na kuutambulisha kwa watu.

Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo wa shirikisho la chama cha kabadi Zanzibar, Abdalla Juma Abeid na Makamu Mwenyekiti wa mchezo huo, Ali Seif Juma, walisema historia inaandikwa kwa kuzindua mashindano hayo kwani haijawahi kufanyika tangu kuanza kuchezwa kwa mchezo huo visiwani Zanzibar.

Walieleza kuwa kuimarika na kuongezeka kwa michezo kunaenda sambamba na juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi za kuwekeza katika sekta ya michezo, na kusema kuwa ligi hiyo ni maalum kwaajili ya kumpongeza kiongozi huyo kwa mageuzia makubwa aliyoyafanya katika sekta ya michezo.

Walifahamisha kuwa timu 12 zitashiriki katika michuano ya mchezo huo zikiwemo timu nne za wanawake ambapo mara baada ya ufunguzi timu ya KMKM wanawake watachuana na Lumumba wanawake, na kwa upande wa wanaume timu ya KMKM na Lumumba zitapimana nguvu.

Viongozi hao walilishukuru Baraza la michezo kupitia Wizara ya Habari kwa msaada wao uliyofanikisha michuano hiyo Kufanyika katika viwanja hivyo na kusema kwao ni fursa ya kuutangaza.

Naifat Ame Hassan na Samir Mubarak Sururu wa timu ya kabadi KMKM walisema wanatarajia kupata ubingwa katika ligi hiyo kwani suala hilo sio geni kwao na wameshafanikiwa katika michezo mingi iliyopita na kupata vikombe.

Aidha wachezaji hao waliahidi kutomwangusha Dk. Mwinyi kwa kuiwakilisha vyema nchi wanaposhiriki mchezo huo ndani na nje ya nchi.

Adam Makame Hamad na Sina Mussa wa timu ya kabadi Lumumba walimshukuru Rais wa Zanziba na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mchango wake unaosaidia kuitambulisha michezo mbalimbali ikiwemo kabadi na kuwashauri vijana kujiunga na mchezo huo kwani utawasiadia kuwatoa kimaisha, na kuimarisha afya zao.

Watazamaji wa michuano hiyo akiwemo Ahlam Khamis walionesha kufurahishwa na mchezo huo na kusema kuwa wanatamani kujiunga.

Michuano hiyo inakwenda sambamba na kauli mbiu " miaka minne ya Dk. Hussein kabadi inajieleza"


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...