MOSHI.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoa wa Kilimanjaro imeokoa fedha milioni 329.4 zilizokuwa zilipie majenereta mawili waliyonunua kupitia kampuni ya Kadco ambayo ni chakavu.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisi za Takukuru mkoa wa Kilimanjaro leo, Naibu Mkuu wa Takukuru mkoa, Sabas Salehe alisema kuwa, matokeo ya ufuatiliaji wa miradi walibaini kampuni ya Kadco kufanya manunuzi ya majenereta mawili kutoka kwa African Power Machinery kwa gharama ya shilingi 329,479,600.

Alisema kuwa, Jenereta zilizowasilishwa zilikuwa na mapungufu kadhaa ikiwa ni pamoja na cable zilizotakiwa kuwa tofauti na zilizowasilishwa aidha injini za jenereta zilikuwa za zamani.

"Baadhi ya maeneo ya jenereta yalikuwa yanakutu na maeneo mengine yalikuwa yamepakwa rangi hivyo Takukuru tulifanya udhibiti juu ya ununuzi wa majenereta hayo mawili na kuzuia malipo kufanyika kwa kampuni iliyosambaza jenereta hizo na kuokoa kiasi hicho cha fedha" Alisema Salehe.

Naibu Mkuu huyo wa Takukuru alisema kuwa, katika hatua nyingine Takukuru ilibaini kusuasua kwa ujenzi wa hospitali ya Manispaa ya Moshi kutokana na kutofanyika malipo kwa wakati kwa Mkandarasi Humphrey Construction Co. Ltd kiasi cha shilingi 213,616,823.

Alisema kuwa, baada ya ufuatiliaji ofisi iliwasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ambapo mnamo Agosti 10 mwaka huu waliweza kumlipa fedha zote na kufanya ujenzi uendelee.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...