Tamasha la Chakula la Coca-Cola Tanzania maarufu ‘Kitaa Food Fest’ limehitimishwa jijini Dar es Salaam kwa kishindo kikubwa huku maelfu ya wahudhuriaji wakifurahi ladha ya vyakula mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.

Tamasha hilo lililofanyika Jumamosi, Novemba 23, katika viwanja vya 710 Kawe, liliambatana na burudani ya muziki, mabalozi mbalimbali wa chapa ya Coca-Cola akiwemo pia mpishi maarufu kutoka Kenya na mcheza Rugby wa zamani Dennis Ombachi, anayejulikana kama ‘The Roaming Chef.’

Tamasha hilo liliwaleta pamoja Mama na Baba Lishe zaidi ya 40 wa hapa nchini ambao waliandaa vyakula mbalimbali za vyakula vya asili ya Kitanzania, vilivyoambatana na vinywaji vya Coca-Cola ili kumalisha mlo. Tamasha hilo lilisifu utofauti na ubunifu wa vyakula vya Kitanzania.

Mpishi maarufu kutoka Kenya Dennis Ombachi, anayejulikana kwa mtindo wake wa kipekee wa upishi na haiba yake inayovutia kimataifa, alikuwa mmoja ya kivutio kikuu katika hafla hiyo.

Ombachi alijiunga na wapishi maarufu wa hapa nchini katika mapishi yaliyoruka moja kwa moja na kuwa kivutio katika kuwahamasisha waliohudhuria kupitia ujuzi wake wa upishi.

“Uwepo wa Dennis Ombachi ulileta msisimko wa kipekee kwenye tamasha la mwaka huu,” alisema Bi. Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Masoko wa Coca-Cola Tanzania. “Ubunifu wake, pamoja na vipaji walivyojaaliwa wapishi wetu wa hapa nchini, vimelifanya tukio hili kuwa la kukumbukwa sana.”Tamasha hilo halikuhusu chakula pekee—lilihusisha burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki pia.

Kwa upande wake Bw. Jonathan Jooste, Kaimu Meneja Mkuu wa Coca-Cola Kwanza, alisisitiza lengo kuu la tamasha hilo: “Tukio hili si kuhusu chakula kizuri pekee. Ni kuhusu kusherehekea utamaduni, mshikamano, na furaha ya watu kuwa pamoja wakifurahia chakula na vinywaji vya Coca-Cola.

Wahudhuriaji mbalimbali walilisifu tamasha hilo kwa kuja kitofauti na kuwaleta pamoja wadau wa chakula kwa njia ya kibunifu.

Akiongea kuhusu mafanikio ya tamasha hilo, Bi. Nshimo aliongeza, “Tunajivunia kufanya Kampeni ambapo wapenda chakula na wapishi wanaweza kuungana, kusherehekea kwa pamoja.


Tamasha la Chakula la Coca-Cola Kitaa Food Fest kwa mwaka huu limeweka viwango vipya kwa matukio ya upishi nchini Tanzania.”Sherehe za tamasha hilo zilizojaa furaha ziliangazia dhamira ya Coca-Cola ya kuwaunganisha watu kupitia chakula na kukuza mahusiano ya kitamaduni yanayozalisha kumbukumbu za kudumu.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...