LEO hii tarehe 25 Novemba Meridianbet inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake Kupitia Kampeni yao ya "PINGA UKATILI, SIMAMA NA MWANAMKE"

Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet, imeungana na dunia nzima kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake, inayofanyika kila mwaka tarehe 25 Novemba ambapo katika kuadhimisha siku hii muhimu, Meridianbet imezindua kampeni maalum ya kijamii ya "PINGA UKATILI, SIMAMA NA MWANAMKE", inayolenga kuongeza uhamasishaji na elimu kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na kuhimiza jamii kuchukua hatua madhubuti za kupambana na vitendo hivi viovu.

Kampeni hii ya "PINGA UKATILI, SIMAMA NA MWANAMKE" inalenga kuhamasisha watu wote, wakiwemo wateja wa Meridianbet na jamii kwa ujumla, kuwa na jukumu katika kumaliza ukatili dhidi ya wanawake.

Katika jamii yetu hii ya leo tumeona jinsi ambavyo wanawake wananyanyasika katika vyanzo vyote vya kiuchumi, jamii, siasa, elimu na kwenye kila kitu hivyo Meridianbet imeamua kuleta kampeni hii ili kudhibiti hili kwa kutoa elimu ya kijinsia.

Lakini pia wakati ukiendelea kuwaza namna ya kupinga ukatili kwa wanawake kumbuka kusuka jamvi lako na Meridianbet leo hii kwani mechi mbalimbali zinaendelea Jumatatu ya leo. Pia unaweza ukacheza michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruit, Super Heli na mingine kibao.

“Lengo haswa la kuja na kampeni hii ilikuwa ni kuwahimiza watu wote kuhusu haki za wanawake na kuhakikisha kuwa wanapata usawa, heshima kwenye jamii na kulindwa pia hasa ukizingatia wanawake wanafanyiwa sana vitendo vya kikatili.” Alisema Nancy Ingram ambaye ndiye Mhariri wa Meridianbet.

Ikumbukwe kuwa kampeni hii pia inatoa nafasi kwa wateja wa Meridianbet na wadau wengine kushiriki kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kutumia mitandao ya kijamii kueneza ujumbe wa kampeni, na kujitolea kwa ajili ya kusaidia kutoa msaada kwa wahanga wa ukatili dhidi ya wanawake. Hii ni hatua muhimu katika kupambana na ukatili, huku ikiwasaidia wanawake kutambua haki zao na namna ya kujilinda.

Meridianbet inawasihi watu wote kuchukua hatua zinazohitajika ili kumaliza ukatili dhidi ya wanawake, na kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na mazingira salama na yenye heshima kwa kila mtu, bila kujali jinsia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...