Serikali ya Tanzania imetoa wito kwa kampuni zinazojihusisha na biashara ya kaboni nchini kujenga uwazi na kuhusisha jamii kwenye maeneo ya miradi ili wananchi wawe nba ufahamu wa biashara hiyo.

Pia, imezitaka kampuni hizo kutimiza ahadi wanazoweka katika biashara ya kaboni ili kuleta manufaa ya kuhifadhi bionuwai na faida kwa jamii.

Wito huo umetolewa na Mhifadhi Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) aliposhiriki mkutano wa pembezoni wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) jijini Baku, Azerbaijan.

Mkutano huo umeandaliwa na Kampuni ya Terraformation wenye mada iliyolenga upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uongoaji wa ardhi na misitu kupitia biashara ya kaboni.

Katika majadiliano hayo, Dkt Elikana alieleza kwa kampuni hiyo kuwa nchi imeweka lengo la kurudishia hekta milioni 5.2. ilikratibiwa na TFS na Ofisi ya Makamu Rais.

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mbalimbali tayari Ofisi ya Makamu wa Rais imeshaandaa Kanuni na Mwongozo wa biashara hiyo ili iweze kuinufaisha jamii.

Ili kufanikisha hayo, Dkt Elikana aliongezea kwa kusema kuwa Tanzania inahitaji uwekezaji na ufadhili wa miradi hiyo kutoka kwa wadau mbalimbali duniani kote.

Halikadhalika, amebainisha kuwa utalaam wa kuandaa miradi hiyo unahitajika pamoja na kufanyika kwa tafiti kwenye maeneo ya misitu ili kuja na matokeo chanya.
Mhifadhi Mkuu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) akizungumza kwenye mkutano wa pembezoni wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) jijini Baku, Azerbaijan.


Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia mkutano wa pembezoni wakati wa Mkutano wa 29 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) jijini Baku, Azerbaijan.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...