Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amefanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara leo Tarehe 14 Novemba 2024 yenye lengo la kukutana na wadau mbalimbali wa sheria mkoani humo.

Akiwa Mkoani Mtwara, Mhe. Johari amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, kwa ajili ya kujitambulisha na kumueleza lengo la ziara yake ambayo ni ya kwanza mkoani humo tangu ateuliwe na Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kushika nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika salamu zake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Patrick Sawala amemueleza kuwa Mtwara iko salama, na Serikali inaendelea kushirikia na wadau wengine kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuwa salama.

Akielezea lengo la ziara hiyo, Mhe. Johari amesema kuwa ni kutembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Mtwara, na kukutana na watendaji wa ofisi hiyo kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za sheria kwa wananchi.

"Mkoa wa Mtwara ni mkubwa na una shughuli nyingi za kiuchumi, hivyo ni vema kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya Ofisi ya AG ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wananchi wengine"

"kama nilivyosema tunaendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo katika ziara hii tunakutana na watumishi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusisitizana juu ya kuwahudumia wananchi" ameeleza Mhe. Johari.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia ametembelea eneo linalotarajiwa kujengwa jengo la Ofisi za Kanda, pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara, iliyopo jengo la Chama cha Waalimu Mkoa wa Mtwara.
 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Hamza S. Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala pamoja na watendaji wengine, baada ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Tarehe 14 Novemba 2024
 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Hamza S. Johari akipokea zawadi ya Korosho kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, alipomtembelea Ofisini kwake leo Tarehe 14 Novemba 2024
 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Hamza S. Johari akisaini kitabu cha Wagane kwenye Ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara, ikiwa ni sehemu za siara yake aliyoifanya leo Tarehe 14 Novemba 2024 Mkoani humo.
 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Hamza S. Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, alipomtembelea Ofisini kwake leo Tarehe 14 Novemba 2024

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...