Na Mwandishi wetu Dodoma

CHAMA cha Mawakili Tanganyika (TLS) ni mdau muhimu katika kuishauri Serikali kwa kubaini mambo muhimu yaliyopo katika utekelezaji wa Sheria mbalimbali nchini hivyo kuna umuhimu mkubwa wakaendelea kushirikiana na Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo Leo tarehe 1 Novemba, 2024 ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa TLS walipofika kwa ajili ya kujitambulisha, kufahamiana na kuboresha mahusiano baina ya Ofisi hizo.

"TLS ni mdau wetu mkubwa hivyo tunathamini sana ujio wenu na tunaamini itaongeza wigo wa ushirikiano katika utendaji kazi"Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa TLS Wakili Boniphace Anyisile Kajunjumele Mwabukusi amesema TLS inaiona Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni nyumbani hivyo pande hizi mbili zinapaswa kushirikiana kwa maslahi ya Wanasheria na Taifa.

"Tunapenda TLS ifanye kazi kwa maadili Uwakili wetu uwe credible tunaweza kushindana na kuvutia watu wa au aina tofauti tofauti kwa kuzungumza na kuimarisha Sheria kwa manufaa ya Taifa letu."Alisema Rais wa TLS

Kwa upande wake Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Samwel Maneno amesema, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sasa imepiga hatua kubwa katika matumizi ya mifumo mbalimbali ili kuimarisha na kurahisisha utekelezaji wa majukumu yake ikiwa ni pamoja na mfumo wa OAG-MIS unaowezesha upatikanaji wa Sheria mbalimbali pamoja na Sheria zote zilizofanyiwa Marekebisho.

Aidha, Naibu Mwanasheria Mkuu amemuomba Rais wa TLS kutumia majukwaa yao kutangaza mafanikio ya mfumo huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...