Na Nasra Ismail, Geita.

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya Geita wametakiwa Kutekeleza miradi ya miundombinu ya barabara zenye changamoto kabla ya msimu wa mvua kuanza pamoja na ujenzi wa madaraja ili kurahisisha Shughuli za maendeleo.

Hayo yamejiri Novemba 14,2024 Katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa siku ya pili katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri -Nzera ambapo Baraza hilo limepokea taarifa za utekelezaji wa Shughuli za maendeleo ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024.

Baraza hilo limepokea taarifa za Kamati za Kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba ambapo Jumla ya Kamati tano zimewasilisha taarifa zake.

Aidha kwa mujibu wa kanuni Na 22 ya kanuni za Halmashauri waheshimiwa Madiwani waliweza kuuliza maswali ya papo kwa papo na kupata majibu katika kamati hizo ambazo ni Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Elimu Afya na Maji, Kamati ya kudhibiti UKIMWI na Kamati ya Maadili.

Katika Kikao hicho, waheshimiwa Madiwani wameiomba ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Geita kutengeneza miundombinu ya barabara zenye changamoto kabla ya msimu wa mvua.

Akizungumza katika Baraza hilo Mhandisi kutoka ofisi ya TARURA, Jerry Mwakapemba amelieleza Baraza hilo kuwa ofisi ya TARURA inaendelea Kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara kulingana na bajeti zake kwa kila mwaka.

Ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inahudumia mtandao wa Barabara za Vijijini (collector feeder and community roads) wenye jumla ya Kilometa 1745.79 zikiwepo barabara za lami km 4.2, changarawe km 655.07 na udongo km 1086.52 pamoja na madaraja 518.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu amewataka TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ili Barabara hizo zitoe huduma kwa Wananchi kuepusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na ubovu wa miundombinu.

Kazungu ameongeza kwa kusema Halmashauri kupitia bajeti zake itatenga kiasi kwa ajili ya kuiongezea nguvu TARURA ili kuendelea kukarabati miundombinu ya barabra kurahisisha shughuli za maendeleo.

Jumla ya Shilingi Bilioni 1.85 kutoka mfuko wa Barabara (road fund) imetengwa kwa ajili ya kufanya ukarabati wa Barabara (maintenance) mfuko wa majimbo ya Geita na Busanda kiasi cha shilingi Bilioni 1 na Tozo ya mafuta kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...