Na. Mwandishi wetu - Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali itaendelea kuwawezesha Wajasiriamali Wanawake na Vijana kwa kuwapatia maarifa, masoko, fursa za kijamii na kiuchumi ili waweze kupiga hatua katika kujenga uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.
Aidha, amesema Wajasiriamali Wanawake ni nguzo muhimu katika kutengeneza Ajira na kukuza uchumi wa maendeleo ya Taifa, hivyo uwekezaji kwao ni kipaumbele cha serikali katika kuhakikisha wanapata nafasi sawa.Mhe. Ridhiwani amebainisha hayo leo Novemba 13, 2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Panda event 2024, ambayo ilikuwa na kauli mbiu isemayo Wawezeshe Wasichana na Wajasiliamali kuvumbua fursa za masoko na kuboresha viwanda
Amesema Serikali imejipanga kutoa sera zinazohimiza uwezeshaji wa kifedha, programu zinazojenga daraja la kidijitali na kuhimiza ushirikiano wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wanawake.












Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...