Na Oscar Assenga,Lushoto
Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ataunda timu maalumu ili kufuatilia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo la Soni katika Halmashauri ya wilaya ya Bumbuli na baade waanze kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo kwa haraka.
Aweso aliyasema hayo wakati alizungumza na wananchi wa Mji wa Soni wilayani Lushoto katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya Soni ambapo Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuhakikisha inatatua changamoto ya huduma za maji kwa wananchi.
Alisema baada ya ufuatiliani huo na majibu ya kamati wataanza kuchukua hatua za haraka Kwa kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo itaondosha tatizo hilo Ili waweze kufanya shughuli nyengine za uzalishaji Mali badala ya kutumia muda kufuata huduma hiyo.
Aidha alisema pia lazima eneo la Soni kuwepo na taasisi ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia huduma ya maji ikiwemo kuanzia Mamlaka ya maji itakayokuwa mwarobaini wa kuondoka na adha wanayokumbana nayo.
"Niwaambie hapa kuna mambo matatu tutayafanya hapa kwanza kuunda timu maalumu itafuatilia na kujua uhalisia wa maji yalivyo ,tuanzishe Mamlaka ya maji katika mji wa Soni lakini tutahakikisha tunajenga mradi wa maji hapa"Alisema
Hata hivyo alimueleza Mkuu wa wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye timu hiyo atakayoiunda itakapofika wilayani humo itafika kuripoti ofisini kwake na baadae kuendelea na shughuli hiyo ambayo itachua muda wa wiki moja
Agizo la Waziri huyo lilitokana na malalamiko ya wananchi katika mji wa Soni ambapo walimueleza kwamba katika baada ya maeneo kuna tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama jambo ambalo wakati mwingine linawapa wananchi wakati magumu.
Akizungumza mmoja wa wananchi hao Shaban Mkufya alisema kutokana na changamoto ya shida ya maji hata wakisikia Soni,Lwandai kuna tatizo la ugonjwa wa kipindupindu wasishangae.
"Mh Waziri hapa Soni kuna mradi ulikuja lakini mabomba hewa hayana maji Lwandai,Soni lakini mpaka Leo wananchi wanapata shida na hasa wanawake ndio wahanga wakubwa na kadhia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...