Balozi wa Marekani nchni Tanzania,  Michael Battle akizungumza alipotembelea Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kufanya kikao cha pamoja kwa lengo la kujenga ushirikiano zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Sikoseli.

Meneja Mradi Programu ya Sikoseli kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) Dkt. Agnes Jonathan akielelezea mikakati ya chuo katika kukabiliana na Ugonjwa wa Sikoseli nchini wakati wa ziara ya balozi wa Marekani nchini Tanzania chuoni hapo Novemba 8,2014 jijini Dar es Salaam.
Mtafiti Mkuu wa programu ya Sikoseli kutoka  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dkt. Irene Minja akielezea namna wanavyopambana kuumaliza ugonjwa wa Sikoseli Nchini wakati wa ziara ya Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Chuoni hapo, iliyofanyika Novemba 8, 2024 jijini Dar es Salaam..

Balozi wa Marekani Chini Tanzania, Michael Battle akisalimiana na Profesa Appolinary Kamuhabwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) wakati ziara ya balozi Battle chuoni hapo Novemba 8,2024 jijini Dar es Salaam 

SERIKALI ya Marekani imeiahidi kuisaidia serikali ya Tanzania kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Sikoseli ili kupunguza ugonjwa huo kama siyo kuumaliza kabisa.

Kauli ya serikali ya Marekani umekuja Wakati takwimu zikionesha kuwa asilimia saba ya watoto wenye umri wa miaka mitano hufariki kwa ugonjwa wa Sikoseli

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle amebaisha hayo Novemba 8,2024 alipotembelea Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na kufanya kikao cha pamoja kwa lengo la kujenga ushirikiano zaidi katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo wa Sikoseli.

“Kuokoa masisha ya mtoto mwenye Sikoseli ni kuikoa jamii na taifa letu litaendeleza ushirikiano kwa ajili ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huo “

Balozi Battle amesema kuwa mashirikiano ya Tanzania na Marekani yanakusudia kuwafanya watoto wenye ugonjwa huo kuwa salama

Amesema, Tanzania ina viongozi mashuhuri wenye ushawishi katika anga za kimataifa ambao wanaweza kuwa mabalozi wazuri kuelekea kumaliza changamoto za ugonjwa huo kwa ujumla.

"Kuna viongozi kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye yeye kwenye medani za kimataifa anaushawishi mkubwa na pia alikwisha wahi kuwa na mgonjwa mwenye tatizo hilo hivyo iko aja ya kumtumia kwani anaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mapambano ya kupunguza ugonjwa huu." Amesema Battle

Pia balozi ameelezea iko haja sasa ya kuzungumza na wazalishaji wakubwa wa viwanda vya dawa duniani ili kupunguza bei ya dawa za Sikoseli au zipatikane kwa unafauu ili kuwapa ahueni wagonjwa wa sikoseli wanategemea dawa hizo za Hydrourea.

Kwa upande wake, Mtafiti Mkuu wa programu ya Sikoseli Dkt. Irene Minja amesema, kuna mipango mbali mbali ya kuhakikisha wanapambana na ugonjwa wa Sikoseli kwa kupunguza makali au kuumaliza kabisa ikiwemo kampeni kubwa ya vunja mduara.

Amesema kampeni hiyo itakuwa ni kuwaelimisha watoto wa shule ambao kabla hawajaanza kuingia kwenye ndoa ili waweze kujijua kama wana vinasaba vya sikoseli kwani karibu asilimia 13 hadi 20 ya watanzania wanavinasaba vya sikoseli.

"Ukiwa na vinasaba na ukakutana na mtu mwingine ambaye naye ana vinasaba basi una nafasi kubwa ya kupata mtoto ambaye nae ataumwa Sikoseli, hivyo tukiwaelisha watoto mapema basi watafanya maamuzi sahihi kwa kupima kabla ili wasipate mtoto ambaye ana Sikoseli jambo ambalo litasaidia kupunguza ugonjwa huo kwa asilimia kubwa na baadae kumaliza kabisa.

Amesema pia kwa sasa wanataka watoto wawe wanafanyiwa uchunguzi mapema ili kuwatambua watoto wenye ugonjwa ili waanze kupata dawa kama Hydroxrea mapema zitakazowazuia kupata maambukizi na kuzia kupata makali ya ugonjwa na tumependekeza hizi dawa zitolewe bure kama ambavyo dawa za ukimwi zinatolewa bure .

Amesema mpak sasa dawa hiyo ya Hydroxrea imeingizwa katika dawa muhimun na hivyo sasa hata bimaya Afya inatoa dawa hiyo.

"Tunataka saizi mambo yabadirike, mwanzo tuliweka nguvu kubwa sana kwenye Ukimwi na baadae tukaweka nguvu kubwa kwenye Korona ilipoingia nchini hivyo sasa njia hizo hizo zitumike kuongeza nguvu kubwa kwenye sikoseli" amesema, kwa sasa nchi za jirani zinafanya tafiti za kutoa vinasaba, na sisi pia tunataka tuingie kwenye hizo tafiti ili wagonjwa wetu pia waweze kufaidika na ikiwa itapatikana tiba nzuri ya vinasaba basi na wao waweze kupata. Amesma Dkt. Minji

amesema kuwa Muhas imewapa madaktari zaidi ya 1000 ujuzi wa kuwalea watoto wenye Sikoseli.

“Tumefanya utafiti itakayowezesha kupata tiba kwa watoto wenye sikoseli , eneo jingineni kutoa elimu kwa sasa tumeweza kutoa elimu kwa madaktrari takribani 1000 nchini mzima watakaosaidia kutoa malezi bora kwa watoto wenye sikoseli.

Dkt. Agnes Jonathan meneja Mradi Programu ya Sikoseli Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) amesema " tumetembelewa na Balozi wa Marekani nchini kwetu ambaye ameonyesha utayari wa serikali yao kutusaidia kupunguza vifo vya sikoseli".

Amesema kuwa takwimu zinaonyesha nchini Tanzania asilimia 7 ya watoto wanye umri wa chini ya miaka mitano wanafariki kwa ugonjwa wa sikoseli huku kila mwaka watoto elfu 11 hadi 14 wanazaliwa wakiwa na gonna huo.

Amesema, asilimia 20 ya watanzania wana vinasaba vya sikoseli na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tano kwa ukubwa wa ugonjwa huu duniani na kwa Afrika ni nchi ya nne .

Amesema jamii bado haijaapata uelewa juu ya ugonjwa sikoseli jambo linalopelekea vifo vingi vinavyotokana na ugonjwa huo.

"Tumeanza kupima watoto wachanga katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza na tunatumaini huduma hii itaenda mbali zaidi. HI itawasaidia watoto kupata matibabu mpema na kwa haraka hydroxrea.

Dkt. Agnes amependekeza kuwa huduma ya upimaji wa ugonjwa huo uunganishwe kwenye huduma za kliniki ya Mama na Mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...