Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA, Anthony Kasore akizungumza  wakati wa kuhitimisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi walioomba kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kwa mwaka wa masomo unaoanzia Januari 2025.

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA  ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imedhamiria kutoa kipaumbele kikubwa katika kudahili wasichana wanaoomba kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vyake, ili kukuza uwiano wa kijinsia na kufikia shabaha ya 50% ya udahili wa wasichana.

Azma hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA, Anthony Kasore, tarehe 19 Novemba 2024, wakati wa kuhitimisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi walioomba kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi katika vyuo vya VETA kwa mwaka wa masomo unaoanzia Januari 2025.

Katika kikao hicho cha siku mbili, kilichofanyika katika Chuo cha VETA Dodoma na kuwahusisha wasajili kutoka vyuo vyote vya VETA nchini, CPA Kasore amesema azma hiyo pia itasaidia kuleta hamasa kwa wasichana na wanawake kwa ujumla kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi, hasa baada ya kuona mafanikio ya wahitimu wa kike.

Amesema, mwamko wa wasichana na wanawake kujiunga na mafunzo ya ufundi stadi bado uko chini kwa baadhi ya fani.

“Mathalani, fani za Uashi, Uundaji na Uungaji Vyuma, Uendeshaji Mitambo Mikubwa na Ufundi Magari, jinsia ya kike bado ni wachache sana, Kwa hiyo kuna haja ya kuweka msukumo.” amesema.

Kikao hicho cha wasajili hao kilikuwa na lengo la kuchagua kwa pamoja wanafunzi kwa njia ya mfumo na kufanya msawazo wa wanafunzi katika vyuo vya VETA ili kuweka uwiano mzuri wa udahili katika vyuo vya VETA.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA, Dkt. Abdallah Ngodu, amesema kupitia kikao hicho wasajili wa vyuo vya VETA wamejengewa uwezo wa kudahili wanafunzi kwa njia ya mfumo na wasajili wapya wamepata fursa ya uelewa wa namna ya kuingiza takwimu na taarifa za wanafunzi wapya kwenye mfumo.
 Baadhi ya washiriki katika uhitimishaji wa zoezi la uchaguzi wa wanafunzi waliomba kujiunga na vyuo vya VETA mwaka wa masomo 2023/2025.
Picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa VETA CPA Anthony Kasore  katika uhitimishaji wa zoezi la uchaguzi wa wanafunzi waliomba kujiunga na vyuo vya VETA mwaka wa masomo 2023/2025.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...