MKuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 20, 2024 wakati wa kutangaza siku ya Mahafali ya chuo cha Kodi yatakayofanyika Novemba 22, 2024.


Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
WAZIRI wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 17 ya Chuo cha Kodi (ITA) yatakayofanyika Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam na kuwatunuku vyeti Wahitimu 417.

 Pia atawatunuku wanafunzi wa vyeti, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo chuoni hapo, MKuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Profesa Isaya Jairo amesema "Pamoja na kutunuku vyeti pia atatoa zawadi kwa wanafunzi wanaobaki chuoni hapa ili kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo yao.Katika idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF)." Amese
ma Jairo

Ameongeza,"Wahitimu 28 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM), 61 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 watatunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT)." Amesema Prof.Jairo.

Prof. Jairo amesema Chuo hicho kinajivunia mafanikio mengi katika utekelezaji wa Mpango mkakati wa awamu ya Tano wa Chuo ambao umejikita katika kutoa mafunzo kwa njia ya kisasa yaani kidijitali.

"Tayari maandalizi ya kutoa elimu masafa kwa njia ya mtandao yameanza na yanaendelea vizuri hivyo itasaidia kupunguza gharama kwa wanafunzi walioko mikoani na kuongeza idadi ya wahitimu kwani mwanafunzi hayakuwa na ulazima wa kusafiri kuja chuo bali kila kitu atapata mtandaoni." Amesema Prof.Jairo

Amesema pamoja na jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa watumishi wa TRA, Chuo cha Kodi vilevile kinatoa mafunzo na ushauri elekezi kwa wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na mamlaka zingine za Mapato Afrika kama vile Sudan, Botswana na Somalia.

Prof. Jairo ametumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kuwa kufanyika kwa mahafali ni fursa nzuri ya kuwapongeza wahitimu pamoja na kutathmini mafanikio na shughuli ambazo zinafanywa na Chuo. Pamoja na kuwaalika wageni kutoka Mataifa mbalimbali ambao ni wadau na washirika katika maendeleo ya taaluma ya forodha na kodi ili kuvutia fursa za uwekezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...