Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimepongeza mchango mkubwa unaotolewa na Mkurugenzi wa shule za Tusiime za Tabata Sanene jijini Dar es Salaam, Dk. Albert Katagira kwa chama hicho mara kwa mara.


Pongezi hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Wazazi, Sudi Kassim Sudi, kwenye kikao chao kilichofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa shule hizo jijini Dar es Salaam.


Sudi alisema Mkurugenzi wa shule hiyo Dk. Katagira ameonyesha upendo  wa hali ya juu na kukiheshimisha chama hicho kutokana na michango yake ya mara kwa mara.


“Mapokezi tuliyopata hapa Tusiime na heshima tuliyopewa tunaahidi kurudi tena kufanya mkutano wetu hapa mwakani, nakushukuru sana tulikuwa na kijana wako na watumishi wengine walitupa ushirikiano wote, kila mara walikuwa wakituuliza tunataka nini,” alisema


“Mwanangu kasomashule hii kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na kwa bahati nzuri kapata daraja la kwanza, hii shule inamaadili ya kiislamu na kikristu, nyie ni mashahidi mmekuja hapa mkiwa na imani ya kiislamu lakini mmesali bila tatizo na wakristo nao wamewekewa mazingira mazuri ya kufanya ibada,” alisema


“Mimi kwa nafasi yangu kama Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa ntaendelea kukutangaza hadi kwenye mikutano ya Baraza Kuu Dodoma kwasababu wewe unatoa fursa kwa chama hicho,” alisema





Mwisho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...