WANANCHI wa Mkoa wa Kilimanjaro wamehiimizwa kutumia Tamasha la asili la kiutamaduni la Kilimanjaro Cultural Festival KCF kujifunza wao pamoja na watoto na vijana kuhusu tamaduni, Mila na desturi za makabila yao ikiwemo vyakula vya asili, viinywaji, faida zake, Lugha za asili na kubadilisha mtazamo wa maisha na malezi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw Nurdin Babu alisema hayo katika bustani ya Kilihome mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro wakati akizindua Tamasha la KCF kwa mwaka 2024 ambapo akataka matamasha ya aina hiyo kutumika kukuza Mila, tamaduni, na desturi na kukuza uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja.
P
Babu alisema utamaduni wa makabila hayo yakiwemo ya wachaga, wamasai, wapare na wengine ulipotea sana lakini kupitia Tamasha hiko wanakwenda kuurudisha kwa maonesho kama hayo ya vinywaji vya asili na vyakula vya asili.
Akaelekeza Tamasha lijalo watoto wa makabila hayo washindanishwe kuzungumza lugha zao ili kuona namna wanavyozifahamu lugha zao kwani imebainika kutokana na watoto wengi kuzaliwa mijini ama kuzaliwa kwenye mchanganyiko wa makabila ya wazazi wamekuwa hawajui lugha zao wala asili zao.
Mkuu huyo wa Mkoa akaahidi Serikali ya Mkoa huo itashirikiana na Kilimanjaro Cultural Festival kuliendesha Tamasha hilo kutokana na umuhimu wake kwa jamii, uhifadhi, utamaduni na kiuchumi
Aidha akasema ni lazima kufanya mambo makubwa Mkoani Kilimanjaro Ili mkoa huo uimarike kwasababu
"hali ya Ulinzi na usalama ya Mkoa ni nzuri ya kutosha kwahiyo lazima tufanye mambo makubwa Ili mkoa uzidi kuimarika"Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu huyo wa Mkoa pia akkawaelekeza waandaaji wa Tamasha hilo kuwasiliana na Katibu Tawala wa mkoa huo Bw Kiseo Nzowa kwaajili ya kuangalia namna nzuri ya kuratibu Tamasha lijalo litakalofua na kuwa lenye tija zaidi.
Aidha akawashauri kuwasiliana na Uongozi wa Manispaa ya Moshi na halmashauri ya Moshi ili kupata maeneo kwaajili ya Ujenzi wa Majengo ya kudumu ya taasisi hiyo na kuongeza zaidi thamani kwani taasisi hiyo iliyoundwa kutokana na kundi sogozi la WhatsApp la watu wanaoishi na kufanya kazi Ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro inaendelea kukua.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Bw Ansi Mmasi alikiri tamasha hilo kuchangia kuhifadhi, kutambua na kurithisha Tamaduni za makabila ya watu wa Mkoa wa Kilimanjaro sambamba na kukuza uchumi wa wananchi.
Mmasi akasema tayari taasisi hiyo imeshatambua na kuandikia maandiko kuhusu vivutio vya kitalii vya kiutamaduni ikiwemo maporomoko ya maji, mahandaki na vivutio vingine ambavyo taasisi hiyo utaendelea kutangaza Ili hata wanaotoka nje ya Mkoa huo wafike kuyatembelea.
"Huko tunataka pia wapate fursa ya kula vyakula vya asili na kulala na wananchi wataona utamaduni ukichangia uchumi wao na wa Taifa , watalala kupitia nyumba zilizo kwenye program ya Kilimanjaro Homestay ambayo pia ilizinduliwa mwaka Jana na taasisi wakilenga kutambua, kuzisajili na kutumia nyumba zinazoachwa kwa muda mrefu na wamiliki ambao hawaishi mkoa wa Kilimanjaro, amesema tayari nyumba zaidi ya 300 zimeainishwa na nyumba zaidi ya 40 zimeshakaguliwa na kuingizwa kwenye program ya kukodishwa kwa malazi kwa madaraja mbalimbali.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw Kiseo Nzowa, alipongeza uwepo wa matamasha hayo kwani jamii yeyote isiyojali na kutambua Tamaduni zao basi hao ni jamii mdu.
.
Mwisho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...