.jpeg)
Mbunifu wa mfumo wa mzunguko wa Sayari alioubuni kwaajili ya kufundishia katika shule za Msingi, Sekondari na taasisi mbalimbali nchini. Akizungumza
MBUNIFU Ernest Maranya kutoka Taasisi ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi nchini(VETA) ametoa ushauri kwa Serikali kuangalia namna ya kuwepo kwa miongozo kwa ajili ya wagunduzi kwani kwa sasa changamoto iliyopo hakuna muongozo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Desemba 02, 2024, wakati wa kongamano la Kisayansi lunalofanyika jijini Das Salaam kwa siku tatu lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Maranya ameeleza kuwa ili kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wanaeleweka kisheria kuna kila sababu ya wadau wa elimu kuhakikisha inakuwa na muongozo kwa ajili ya wabunifu.
Katika maonesho hayo Maranya ambaye amekuwa akionesha kifaa alichobuni kinachotoa elimu ya anga amesema pia ipo haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuharakisha elimu ya anga kwa kutumia mfumo unaofanya kazi zaidi kukiwepo na Sumaku na ili utumike katika shule zote.
Amesema anaiomba Serikali na wadau wa elimu nchini kuhakikisha wanaendelea kumuunga mkono katika kufanikisha ubunifu wake unafika maeneo yote nchini.
Amesema pamoja na kugundua mfumo huo na kukubalika lakini bado msukumo wa kuruhusu kuanza kutumia mashuleni bado ingawa anashukuru wadau wa elimu wamekuwa waliofika kwake kujifunza na kualikwa kwenye baadhi ya shule kuuelezea kwa wanafunzi.
Pamoja na mambo mengine Maranya amesema kuna shule za binafsi zaidi ya 30 ambazo ametembelea kutoa elimu hiyo lakini kunaugumu kwenye shule za serikali jwa sababu hakuna mwongozo wa kuzifikia shule hizo.
Pia Maranya ameeleza kuwa tayari ameshaandika baadhi ya miongozo lakini bado

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...