Jumla
ya wanafunzi wa kike 2600 wamejengewa uwezo wa masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Kampuni ya simu ya Mikononi ya
Vodacom Tanzania tangu 2018 mpaka mwaka huu kupitia program ya Code Like
a Girl
Mkuu wa Kanda ya kati wa Vodacom Tanzani, Joseph Sayi
alisema hayo leo desemba 13 wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya
TEHAMA yaliyofanyika Chuo kikuu cha Dodoma (Udom).
Alibainisha
kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa awamu kwa baadhi ya Mikoa
hapa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa masomo ya Sayansi,
Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) wanafunzi hao wa kike kwa
ufadhili wa Vodacom Tanzania PLC.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule za sekondari Kanda ya kati wakijifunza jinsi ya kutumia kopyuta kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA ) yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...