Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya wenye ulemavu Tanzania Jonas Lubago (katikati) akizungumza katika kongamano la kuelekea siku ya Walemavu duniani  lililoandaliwa na Shirika la Afya ya uzazi la Maria Stopes Tanzania (MST) kulia kwake ni Kagemuro Rujoro Afisa Ustawi wa Jamii wa jiji la Dar es Salaam na kushoto ni Oscar Kimaro Mkuu wa Idara ya Uchechemuzi  (MST)

Afisa Ustawi wa Jamii wa jiji la Dar es Salaam Kagemuro Rujoro,  akizungumza Waandishi wa Habari kuelelekea maadhimisho ya siku ya Walemavu nchini. Ambapo pamoja na mambo mengine walemavu kutoka sehemu mbali mbali nchini wamepatiwa elimu ya Uzazi kutoka shirika la Afya ya uzazi la Maria Stopes Tanzania (MST). Maadhimisho siku ya walemavu duaniani huadhimishwa Deaemba 3, kila mwaka.
Tungi Mwanjala Mlemavu ya kusikia, akitoa ushuhuda katika kongamano hilo  namna alivyopata changamoto alipoenda Hospitali kujifungua.

Oscar Kimaro Mkuu wa Idara ya Uchechemuzi kutoka shirika la Afya ya uzazi la Maria Stopes Tanzania (MST)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika kongamano liliandaliwa na Maria Stopes kuelelekea maadhimisho ya siku ya Walemavu nchini. Ambapo pamoja na mambo mengine walemavu kutoka sehemu mbali mbali nchini wamepatiwa elimu ya Uzazi kutoka shirika la Afya ya uzazi la Maria Stopes Tanzania (MST). Maadhimisho siku ya walemavu duaniani huadhimishwa Deaemba 3, kila mwaka



Serikali Yaendelea Kuboresha Mazingira Ya Kutoa Huduma Za  Afya kwa Walemavu

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

SERIKALI kupitia Ofisa wa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam imesema kuwa itaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuondosha unyanyapaa kwa walemavu pamoja na kuendelea kuboresha mfumo wa kutoa huduma ya afya hususan ya uzazi kwa walemavu.

Hayo yamesema  Desemba 2, 2024 na Kagemuro Rujoro Ofisa Ustawi wa Jamii wa jiji la Dar es Salaam aliyemwakilisha Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani.

Kagemuro amesema kuwa tayari serikali ishapiga hatua kwa kuweka wakalimani wa lugha za alama na walewanaowezakuzungumza na watu wenye aina mbalimbali za ulemavu kwenye vituo vya kutoa huduma ya afya kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma bora.

“Tutaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala unyanyapa kwa walemavu ili kupunguza hali hiyo” alisema.

Kwa upande wake, Oscar Kimaro Mkuu wa Idaraya Uchechemuzi katika shirika la Afya ya uzazi la Maria Stopes Tanzania (MST) amesema wanatambua na kusisitiza umuhimu wa haki za msingi za watu wenye ulemavu hivyo watahakikisha wanaitumia siku hiyo wanaitumia kwa  kutoa wito juu ya msingi mzima wa kuendelea kupata haki muhimu, hasa hasa ya uzazi.

 “Pili tunaendelea kutoa msisitizo kwa watunga sera na wafanya maamuzi mbalimbali kuendelea kuweka msisitizo wa namna ya kufikisha huduma na taarifa sahihi ya huduma ya afya ya uzazi kwa walemavu wote awe wa kusikia , kuona , kutembea au wa kuzungumza”

Ametaja changamoto zinazowakabili walemavu ikiwa pamoja kukosa viti mwendo vya kuwafikisha kweneye vituo pia kukosa mawasiliano baina ya mtuo huduma na mlemavu hususan walemavu wa kusiki ama wa kuona.

‘kwenye jasmii kuna unyanyapaa utasikia watu huwaambia watu wenye ulemavu wenye ujuzito kuwa hawajionei huruma kubeba mimba katika hali ya ulemavu wanasahasu kuwa hawa ni bindamu wanstahili sawa”

Amesema kwa kufanya hivyo kutakuwa kuna usawa licha ya kundi hilo kuwa kubwa kwenye jamii .

Amesema kuwa takwimu za dunia inaitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi yenye walemavyu wengi ambapo asilimia 11 ya watanzania Milioni 61 ni walemavu 


Naye Jonas Lubago, Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama vya wenye ulemavu Tanzania amesema walemavu wengi wamekuwa wahanga wa afya ya uzazi kwa sababu taarifa au elimu ya Afya ya uzazi kwao imekuwa haiwafikii na mara nyingine wanaipata kwa kuchelewa

Amesema kufuatia hilo baadhi yao wamekuwa wakipata changamoto nyingi ikiwemo kupata watoto wengi ambao wanashindwa hata kuwahudumia  na wengine kulea watoto peke yake huku pia wengine wakidondokea kupata magonjwa ya kujamiiana na hata Ukimwi.

Amesema katika jamii za wenye ulemavu wanawake ndio huathirika zaidi na suala ya afya uzazi hivyo ni vema wakapatiwa elimu mapema.

"Katika kongamano hili tulilenga zaidi wanawake ndio wapate elimu hii kwani katika jamii zetu za wenye ulemavu wanawake ndio huathirika zaidi na suala ya afya ya uzazi... wakina mama wanajukumu kubwa zaidi kwenye afya ya uzazi kuliko wanaume hivyo tukianza na wakina mama tutatakuwa tunatatua tatizo hili kwa upana zaidi" amesema

Aidha ameongeza kuwa  "elimu hii inaumuhimu wake changamoto zilizopo sisi hatujui sana taratibu hizi nzima za uzazi, namna ya kulea mtoto, kupata mtoto na nyingine nyingi ili kupunguza Mimba zisizotarajiwa na pengine kupata mtoto mwenye ulemavu 

"Watu wengine wanadhani mtu mwenye ulemavu hana hisia za mapenzi,  siyo kweli, hisia tunazo na tuna haki ya kuwa na wenza. Mafunzo haya yatatusaidia kuondoa dhana potofu kwa jamii juu ya muonekano wao kwa walemavu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...