Shenzhen,  China: Kampuni ya Huawei kwa mara nyingine tena imedhihirisha dhamira yake ya kuwawezesha vijana wenye vipaji katika nyanja za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kwa kuandaa Kambi ya Utafiti wa Vipaji vya Kidigitali ya Huawei kutoka  katika nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara LEAP lililofanyika kuanzia Novemba 18 hadi 22, 2024 nchini China .

Mpango huo wa kidijiti umedhamiria kutoa maarifa ya Uongozi, na kutoa uwezekano wa fursa za kuajiajiri  ukilenga zaidi kukuza stadi za juu katika tasnia ya kidijitali na kukuza uvumbuzi miongoni mwa vipaji vya vijana kutoka kanda ya Afrika.
 
Kambi hiyo,  iliyofanyika katika makao makuu ya kimataifa ya Kampuni ya Huawei huko Shenzhen, ni sehemu ya dhamira pana ya kuendeleza wafanyakazi wenye ujuzi  katika anga za kidijitali kote barani Afrika, ambayo iliwaleta pamoja wanafunzi wenye vipaji vya kipekee  kutoka nchi 17 za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni pamoja na Tanzania, Nigeria, Afrika Kusini. Mauritius, Kenya, na zinginezo.
 
Kambi hiyo ya utafiti iligusa ajenda muhimu za kidijitali ikijumuisha kozi za ICT  kuhusu teknolojia ya kisasa kama vile Akili Mnemba  (AI), mawasiliano ya mtandao wa 5G, nguvu za kidijitali, teknolojia za masafa  pamoja na kongamano la uongozi. 
Tukio hilo la wiki moja lilifikia  kilele  kwa kuandaliwa shindano la Tech4Good, ambapo washiriki kutoka nchi tofauti waliunda  timu ili kuja na majawabu kupitia teknolojia yanayojibu changamoto  za kijamii.
 
Tanzania iliwakilishwa  na wanafunzi 10 bora kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT). Ambapo Huawei ilitoa ufadhili kamili kwa safari za ndege za kwenfa na kurudi, malazi, na mafunzo kwa washiriki wote, ili kuhakikisha kwamba umakini wao unabaki kwenye kujifunza .

Kambi ya Utafiti wa Vipaji vya Kidijitali ya LEAP, ilizinduliwa na Huawei katika  nchi  za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara mnamo mwaka 2022, ikiwa ni sehemu ya mpango wake mpana wa kukuza wafanyakazi  wenye ujuzi  katika anga za kidijitali kote barani Afrika. 

Huawei inatazamiwa kuinua dhamira yake ya kuendeleza vipaji vya kidijitali katika Afrika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo kwa vijana 150,000 kupitia mpango wake wa kukuza ujuzi wa kidijitali wa LEAP katika miaka mitatu ijayo. 

Mpango huo ni sehemu ya mkakati mpana wa Huawei wa kuwekeza katika rasilimali za kimataifa zinazolenga kukidhi mahitaji mahususi ya vipaji vya kidijitali vya jumuiya za wenyeji.
 
Mpango wa LEAP umeundwa ili kuziba pengo la ujuzi wa kidijitali katika nchi za Afrika  zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa kutoa mafunzo na nyenzo za kina. Ikilenga katika kukuza uongozi wa kidijitali, kujenga wafanyakazi wenye ujuzi wa ICT, kuunda kundi la vijana wenye vipaji vya kidijitali, na kuimarisha ujuzi wa kidijitali miongoni mwa wananchi. Kwa kufanya hivyo, Huawei inalenga kuleta athari kubwa kwenye uwezo wa kidijitali na matarajio ya siku za usoni za nchi za Afrika zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...