MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) FREEMAN Mbowe amewasihi viongozi watakaoshika nyazifa mbalimbali katika Chama hicho ni lazima wakijenge chama katika misingi ya maadili na Nidhamu.

Ameyasema hayo leo Januari 21, 2025 wakati anafungua Mkutano Mkuu wa chama hicho unapendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam.

"Mtakaopewa mikoba ya chama hiki ni lazima mkarekebishe, inawezekana tukavumilia matusi kipindi hiki cha chaguzi lakini msingi wa Chadema sio matusi watakaokabidhiwa mikoba leo wakasafishe"

"Hiki chama tunawajibu wote wa kukilinda kwa gharama yoyote ile na chama hiki tutakilinda". Ameongeza.

Amesema kuwa Chadema kitamaliza uchaguzi wakiwa wamoja na kwamba uchaguzi huo sio vita.

"Uchaguzi huu haupaswi kuwa vita unapaswa kuwa ujenzi ya Demokrasia, Wapo watabiri wengi walisema kuhusu Chadema , Mheshimiwa Mbowe mnakwenda kukipasua Chadema " amesema Mbowe.

Amesema kuwa Chadema kimebeba Ndoto ya Taifa sio Ndoto ya kiongozi mmoja mmoja na wataendelea kupita katika mabonde na milima lakini kila mmoja awe na wajibu wa kukilinda Chadema na njia ya kukilinda ni kuwa na hekima na Nidhamu.

"Kazi tunayowaachia warithi wa chama hichi ni kujenga misingi ya maadili na Nidhamu , matusi sio msingi wa Chadema " amesema Mbowe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...