Mkurugenzi wa Taasisi ya Baobab Shani Khalfan Swai watano kutoka kushoto aliyesimama katikati akiwa na Viongozi wa Bodi ya Uongozi wa Taasisi hiyo kwenye picha ya pamoja.

Na Khadija Kalili Michuzi Tv 
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani  linamshikilia  mtu mmoja (jina kapuni) kwa kosa la  kusambaza  picha  mjongeo kwenye mitandao ya kijamii  kwa  lengo la kuichafua Shule ya Sekondari BAOBAB  iliyopo Wilayani  Bagamoyo Mkoani Pwani.

 Akizungumza  na Waandishi  wa Habari  leo tarehe 20 Januari kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jeshi  la Polisi  Pwani Kamishna Msaidizi  wa Polisi Salim Morcase amesema kuwa  Januari  3 ,2025 walipokea  malalamiko  kutoka  kwa uongozi wa  shule  ya Baobab  kuhusu kusambazwa picha  chafu  katika mitandao  ya kijamii picha za mjongeo za utupu na zenye maudhui  machafu kimaadili na kinyume  na sheria  za nchi.

"Picha  hizo chafu na zisizo  na maadadili  imebainika kuwa  waliotengeneza  waliunganisha na  baadhi ya majengo  ya Shule ya Baobab  ili kuaminisha  umma  kuwa  vitendo hivyo  vinafanyika shuleni hapo" .

 Morcase amesema kuwa  Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani  limefanya  uchunguzi  na limefanikiwa kumkamata mtu mmoja  ambaye  uchunguzi wa kitaalam unesaidia kumfikia na kumkuta  na picha hizo  na kifaa cha kieletroniki ambacho alikuwa akikitumia  kusambaza picha hizo chafu.

ACP Morcase amesema  kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea kuwasaka  watu wengine walihusika katika kutengeneza  na kusambaza picha mjongeo.

RPC Morcase amesema kuwa Jeshi la Polisi Pwani  wanatoa onyo  kwa watu  wenye tabia  kama hizo  za kutengeneza  na kusambaza picha  kama hizo  kwa malengo  ya kuchafua wengine au  taasisi kwani mkono wa sheria lazima  utawafikia na hata  kama  hautawafikia mapema  wataendelea kupata  shida ya kujificha  na kuacha  kufanya  shughuli zao za kujiletea maendeleo 
 Wakati huohuo  Mkurugenzi wa Shule ya Baobab  Shani Khalfan Swai  amesema  kuwa taarifa hizo zimewaathiri kwa kiasi  japo muitikio wa wazazi  kupeleka  wanafunzi Shuleni  hapo ni mkubwa.

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Baobab  Swai amesema kuwa  kusambaa kwa picha hizo chafu za mjongeo  ziliwapa taharuki kubwa  wao uongozi wa shule  pamoja na wazazi kwani simu zilikua za moto jambo lililowafanya waamue kukaa kimya huku wakitafakari njia sahihi ya kujisafisha  na kubainisha ukweli  ndipo walipotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambao wanauwezo wa kufanya uchunguzi  na jambo la kushukuru kwa upande wao waliposikia mtu mmoja mwenye nia ovu anashikiliwa na Jeshi hilo huku uchunguzi ikiendelea. 

Swai ameongea kwenye mkutano  na Waandishi wa Habari waliofika Shuleni hapo.

"Sisi Baobab  tunaimani kubwa na Jeshi la Polisi kwamba wataisafisha Taasisi  yetu iliyochafuliwa.

"Wazazi wa wanafunzi walipatwa na taharuki  wengi walipiga siku kuhitaji kupewa ufafanuzi  na sisi tuliwafafanulia kwamba hakuna tabia chafu hapa shuleni kwetu na hata zile picha mjongeo wale siyo wanafunzi wetu japo kuna picha za mahafali mdukuzi alizidukua akaunganisha na kwa upande mwingine mazingira ya mabweni yako tofauti na ya kwetu sisi" amesema  Swai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...