*Asema mchango wa Aga Khan wa kuigwa katika kusaidia jamii

Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL Company Ltd Altaf Hiran amesema kuwa kifo Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan amejifunza namna ya kuenzi kuipenda jamii katika kuisadia

Hiran ameyassma hayo mara baada ya kusaini kitabu Cha maombolezo ya kifo Mtukufu Hi The Aghakan katika ofisi za Aga khan zilizopo Oyster Bay jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kuwa Mtukufu Aga Khan aliipenda jamii ya katika kutoa mchango wake ambao umesaidia katika kutatua changamoto zilizokuwa zinaizunguka jamii.

Aidha amesema kuwa amesema kuwa matendo yake aliyafanya katika uhai wake ndivyo unavyotaka dini ya kiislaam.

*Kifo cha Mtukufu Aga Khan nitakienzi kwa vitendo katika kusaidia jamii inayonizunguka kwa kile ambacho ninacho kukitoa na kuwa sehemu ya kutatua changamoto"amesema Hiran

Kiongozi Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88 jijini Lisbon, Ureno, Februari 4, 2025.

Mtukufu Aga Khan, anayefahamika kama Karim Al-Hussaini Aga Khan IV, alijulikana kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha ustawi wa binadamu kupitia miradi mbalimbali duniani.

Amesema Katika maisha yake, Aga Khan IV alisisitiza Uislamu ni imani inayohimiza kujitolea, uvumilivu, na utu wa mwanadamu.

Mbali na uongozi wa kidini, alihimiza maendeleo ya jamii kupitia sekta za afya, elimu, habari, utamaduni, na ustawi wa jamii.

Alianzisha miradi kama Shule na Chuo Kikuu cha Aga Khan, Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Aga Khan (AKFED), na Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), ambao umeleta maendeleo katika afya, elimu, na uchumi, hasa Afrika Mashariki.
Nchini Tanzania,
 

Mkurugenzi wa kampuni ya MOIL Company Ltd Altaf akisaini kitabu cha  maombolezo  Kiongozi  Mkuu wa 49 wa Madhehebu ya Shia Ismailia na mwanzilishi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), Mtukufu Aga Khan katika ofisi  za Aga khan zilizopo Oyster Bay jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...