Na Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari,Jerry Silaa amewataka wananchi wanaotapelewa kwa njia ya mitandao ya simu kutoa taarifaa katika mamlaka husika ili hatua kali zaidi zichukuliwe ili kukomesha utapeli huo

Alitoa rai hiyo jijini Arusha Februari 21,2025 katika mkutano maalumu na waandishi wa habari kuhusu kampeni kabambe ya "SITAPELIKI "inayolenga kutoa elimu kwa jamii

Waziri Silaa anasema wananchi wanaotapeliwa watoe taarifaa zao kwa Jeshi la polisi lakini pia kwa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)

"Endapo wananchi watatoa taarifaa polisi mamlaka husika itafanya jitihada za kawasaka matapeli wanaofanya utapeli kupitia simu

Pia amesisitiza kwa wadau wote wa vyombo vya habari kushiriki katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya kampeni ya "SITAPELIKI" ambayo ni kampeni endelevu itakayokwenda kudhibiti vitendo vya utapeli na ulaghai kupitia mitandao.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...