NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
WAWEKEZAJI zaidi ya 40 kutoka nchini Italy na Tanzania wanatarajiwa kushiriki katika Kongamano la nne la Biashara na Uwekezaji la kukuza biashara na uwekezaji ambalo litafanyika Februari 11 hadi 12 katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo linatarajiwa kuvutia ushiriki wa mamlaka kutoka Tanzania na Italia, mashirika ya sekta binafsi, mitandao ya biashara ya kikanda na vyama vya ushirikia.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Februari 3, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa uhamasishaji uwekezaji kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), John Mnali amesema kongamano hilo litaangazia fursa za uwekezaji ambazo hazijatambulika na kutumika kikamilifu nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Teknolojia za kilimo (Agro-tech) na uchumi wa buluu ikihusisha utaalamu kwenye masuala ya mbolea, mifumo ya umwagiliaji, ufugaji, matumizi ya ngozi, ufugaji wa samaki na usambazaji.
Aidha amesema mahusiano ya kiuchumi kati ya Italia na Tanzania yameendelea kukua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.
"Biashara baina ya nchi hizi mbili zimeimarika kwa kiasi kikubwa katika sekta mbalimbali, zikiwemo viwanda, kilimo, utalii, ushirikiano wa kiufundi, mashine, kemikali, vifaa vya umeme, madawa na bidhaa za chakula". Amesema
Amesema kuwa Tanzania inasafirisha bidhaa za kilimo, madini na maliasili kama vile kahawa, chai, pamba, samaki na vitu vya tahamani kwenda Italia.
Naye Balozi wa Italia Nchini Tanzania, Giuseppe Coppola amesema Nchi ya Italia imeonyesha nia kubwa ya kuwekeza Tanzania hasa katika sekta za utalii na kilimo na uwekezaji huo umechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania katika miundombinu ya kilimo, utalii, nishati mbadala na ujenzi wa miundimbinu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...