KAMPUNI ya Airtel Africa, inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano na huduma za kifedha kwa njia ya simu inayopatikana katika nchi 14 barani Afrika, imeahidi kusaidia kutoa mafunzo ya ujuzi wa kidigitali na teknolojia kwa vijana 25,000, wanaotoka katika maeneo 80 katika ngazi ya serikali za mitaa nchini Nigeria.

Msaada huo utatolewa kupitia programu iitwayo ‘3 Million Technical Talents’, iliyotokana na mamlaka ya raisi kwa lengo la kuwapa vijana ujuzi wa kidijitali na teknolojia.

Airtel ilitangaza kuwa itadhamini masomo kwa wanafunzi 10 watakaoenda kusoma masomo yanahusiana na teknolojia kwenye chuo kikuu cha Plaksha nchini India chini ya programu ya uanazuoni ya Airtel Africa. Udhamini wa masomo hayo ambayo unasimamiwa na Airtel Africa Foundation utawapatia vijana ujuzi wa kidijitali na teknolojia sambamba na kuimarisha malengo ya kuziba ufa wa vipaji kwenye sekta ya teknolojia huku ikiendelea kuunga mkono maono ya kulifanya taifa hilo kuwa kitovu cha teknolojia duniani.

Ahadi hizi za kuendeleza viongozi wa baadaye wa teknolojia wa Nigeria zilitangazwa wakati Mwenyekiti wa Airtel Africa, Bw. Sunil Bharti Mittal, KBE na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Africa, Sunil Taldar walipokutana na Rais wa Nigeria, MHE. Rais Bola Ahmed Tinubu wakiwa Ikulu jijini Abuja.

Kwenye mkutano huo pia walijadili uwekezaji unaoendelea wa Airtel Afrika katika sekta ya mawasiliano na uchumi wa kidijitali wa Nigeria.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Bw. Sunil Bharti Mittal alisema: “Nigeria inasalia kuwa soko la kimkakati kwa Airtel Afrika, na tumejitolea kikamilifu kuunga mkono ajenda ya serikali ya mabadiliko ya kidijitali. Kupitia mipango kama vile Airtel Africa Fellowship na uwekezaji wetu katika 3MTT, tunahakikisha kwamba vijana wa Nigeria wanapata elimu ya kiwango cha kimataifa na ujuzi wa kidijitali. Tunapongeza maono ya Rais Tinubu ya Nigeria iliyoendelea kiteknolojia na tumejitolea kutekeleza sehemu yetu katika kufanikisha maono hayo.”

Huku akibainisha kazi kubwa inayoendelea hivi sasa kupitia Mpango wa Elimu wa Airtel-UNICEF Reimagine Education ambao umeingiza shule 1,260 na zaidi ya wanafunzi 600,000 nchini kwenye mifumo ya kidijitali ya kujifunza kama vile Nigerian Learning Passport (NLP), Bw. Mittal alirejelea ari ya Airtel Africa katika upanuzi wa mtandao, ubora wa huduma, na ujumuishaji wa kifedha.

Airtel Africa ilikaribisha uteuzi wa hivi karibuni wa miundombinu ya mawasiliano kama Miundombinu Muhimu ya Kitaifa ya Habari (CNII), ikitambua kuwa ni hatua muhimu katika kulinda na kupanua msingi wa kidijitali wa Nigeria. Pia ilisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuendesha ujumuishaji wa kifedha kote Nigeria, haswa kupitia kampuni yake tanzu, SmartCash PSB.

Bw Taldar alisisitiza lengo endelevu la Airtel kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuharakisha uchumi wa kidijitali wa Nigeria, akisema: “Airtel imewekeza sana katika mustakabali wa kidijitali wa Nigeria. Tunapanua mtandao wetu, kuendeleza ujumuishaji wa kifedha, na kutengeneza fursa kwa wananchi wa Nigeria kupitia teknolojia na uvumbuzi. Ushirikiano wetu na serikali kupitia mipango kama vile Airtel Africa Fellowship na 3MTT inahakikisha kwamba Nigeria inasalia kuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya kidijitali barani Afrika.

Airtel Afrika inaendelea kujidhatiti kushirikiana na serikali ya Nigeria na wadau wengine kwa ukaribu kuendeleza muunganiko wa mawasiliano, maendeleo ya mafunzo ya kidijitali na ujuimuishwaji wa kifedha ili kuimarisha nafasi ya Nigeria kama kinara wa Afrika kwenye Uchumi wa kidijitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...