Ambapo washindi watano wamejishindia TZS 500,000 kila mmoja katika droo ya Tap Kibingwa, ikiendelea kusherehekea hatua ya Tanzania kuelekea uchumi usiotegemea pesa taslimu.


Benki ya Stanbic imeendelea kuwazawadia wateja wake ambao wanatumia huduma za kibenki kupitia Kadi za Visa Debit, huku droo moja ya mwisho ya mwezi ikitarajiwa kufanyika mapema mwishoni mwa mwezi Machi, ikiwa ni droo ya mwisho ya kampeni hiyo.


Droo kubwa ya mwishoni mwa mwezi Machi itamshuhudia mshindi mmoja akiibuka na gari jipya aina ya Suzuki Fronx 2024, zero mileage, ikidhihirisha dhamira ya Stanbic ya kukuza huduma ya benki kidijitali.

Dar es Salaam, Tanzania – Machi 2025 – Benki ya Stanbic imefanikiwa kuendesha droo ya pili ya mwezi ya kampeni yake ya Tap Kibingwa, ambapo wateja watano wamejishindia kiasi cha TZS 500,000 kila mmoja. Kampeni hii inalenga kuchochea matumizi ya Kadi za Visa Debit kwa ajili ya miamala ya kidijitali, ikiendelea kuhamasisha urahisi na usalama wa malipo yasiyo ya pesa taslimu kote nchini Tanzania.

Washindi wa droo ya Machi ni:
Richard Muyambo
Alice Frank Mutagonda
Saddam Ally
Nabbila Abbasali Hirji
Siddharth Misra

Meneja wa Kutoa Kadi wa Benki ya Stanbic, Irene Mutahibirwa, amesisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendeleza malipo ya kidijitali nchini Tanzania.

"Tap Kibingwa ni sehemu ya mkakati wetu mpana wa kuimarisha ubunifu wa kifedha na ujumuishi wa kifedha. Miamala ya kidijitali huleta usalama na ufanisi, na tunafurahia kuendelea kuwazawadia wateja wetu kwa kufanya maamuzi bora ya kifedha," alisema Mutahibirwa.

Tap Kibingwa ni kampeni maalum inayoendeshwa na Benki ya Stanbic inayohamasisha wateja kutumia Kadi za Visa Debit kwa malipo ya kila siku badala ya pesa taslimu. Wateja wanaofanya miamala ya angalau TZS milioni 5 kwa mwezi wanapata nafasi ya kushiriki kwenye droo za kila mwezi. Kampeni hii inaendelea hadi mwisho wa Machi 2025, ambapo droo kubwa itamshuhudia mshindi mmoja akiibuka na gari jipya aina ya Suzuki Fronx 2024, zero mileage.

Kupitia Tap Kibingwa, Benki ya Stanbic inaendelea kudhihirisha dhamira yake ya kukuza ujumuishi wa kifedha na uvumbuzi wa kidijitali, kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma za benki zilizo salama, rahisi, na zenye manufaa. Katika safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kidijitali, benki inawahamasisha wateja wengi zaidi kutumia kadi zao kwa malipo na kujipatia fursa ya kushinda zawadi nono katika droo zijazo.

Meneja wa Kitengo cha Kadi kutoka Benki ya Stanbic, Irene Mutahibirwa (katikati) akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa droo ya pili ya kampeni ya "Tap Kibingwa" inayohamasisha wateja kutumia kadi za Visa Debit. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es salaam na jumla ya washindi 5 walipatikana kwa kujishindia kiasi cha Tsh 500,000 kila mmoja . Wengine katika picha ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Irene Kahwili (kushoto) na Joan Muro, kutoka kitengo cha kadi cha Benki ya Stanbic

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...