Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB )Dkt. Mboni Ruzegea amesema katika kipindi cha miaka minne (2021 - 2025) ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Bodi imeweza kujenga na kuboresha Miundombinu, Ununuzi wa Vitabu ,Vifaa vya ujifunzaji pamoja na uanzishaji wa Maktaba Mtandao Jumuishi ya Kitaifa.
Hayo ameyasema Dkt. Mboni wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya Miaka Minne ya Bodi hiyo kwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Dkt.Mboni amesema mafanikio ya bodi yametokana na serikali kutoa fedha katika kujenga miundombinu ambapo imefanya kuwa kasi katika kutoa huduma za maktaba nchini.
Amesema mafanikio mengine nj kufanya Maboresho ya Sheria ya TLSB, Maandalizi ya Sera ya Taifa ya Huduma za Maktaba na Maendeleo ya Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS).
Aidha ameongeza kuwa, TLSB iko mbioni kuanzisha Maktaba za jamii ambazo zitaenda kuziba mwanya uliopo na kuwawezesha watu waishio maeneo ya pembezoni mwa miji na vijijini kunaufaika na huduma za Maktaba na kujiongezea maarifa na elimu.
Mkutano huo umehudhiriwa pia na Menejimenti ya TLSB, Wakutubi wa Mikoa na watumishi wengine wa TLSB,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...