Na Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa kuwasha Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka utawashwa Mkoani Hapa umefikia asilimia 96.

RC Kunenge amesema hayo leo tarehe 25 Machi 2025.

Kama jinsi mnavyoona Uwanja umependeza tumeotesha majani na kutengeneza majukwaa manne ikiwa ni pamoja na jukwaa la VIP katika

Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha Pwani.
RC Kunenge amesema kuwa mambo yanazidi kwenda kama vile yalivyopangwa.

"Tumetengeneza miundombinu ya maji , umeme na pia tumeweka taa ambazo zitatumika hata baada ya sherehe za kuzindua kuwasha Mwenge wa Uhuru uwanja utatumika kwa shughuli mbalimbali.

Wakati huohuo ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na Mikoa jirani wajitokeze kushiriki katika uzinduzi huo ambapo wanatarajia watu 16,000kuhudhuria.

Uzinduzi huo umepangwa kufanyika tarehe 2 Aprili 2025.

"Kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka huu inasema "Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu" amesema Kunenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...