*Ni kwa wateja watakao jaza gesi katika kipindi cha mfungo
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Oryx yashusha neema katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma kwa wateja wake wataojaza gesi ya majumbani kupata zawadi ya futari ya Tambi ,Sukari pamoja maziwa ya Nazi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Oryx Futari Kunoga,Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Oryx Shaban Fundi amesema kampuni hiyo inafanya utoaji wa futari kwa mifungo ya Ramadhan na Kwaresma ikiwa ni kurudisha kwa jamii.
Amesema kuwa zawadi hizo ni nchi zima kwenye maduka ya kampuni ya Oryx pamoja na maduka mengine yaliyodhibitishwa.
"Tumejipanga kuwafikia wateja wetu katika kipindi hiki kupata zawadi ya futari pindi watakavyojaza gesi kuanzia kilogram sita na kuendelea na neema hii sio ya kukosa"amesema Fundi.
Aidha amesema kuwa zawadi ya Futari Kunoga ni kwa kipindi cha mfungo na hakuna mtu atakaye jaza gesi ya kupikia majumbani akakosa zawadi hizo.
Fundi amesema kuwa uhamasishaji wa matumizi ya Nishati safi ya Kupikia Oryx inaendelea ikiwa ni kuwafikia watanzania wote ili kufikia lengo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...