Na Mwandishi Wetu

Jubilee Health Insurance imesema inayofuraha kutangaza mafanikio yake makubwa nchini Tanzania baada ya kupata tuzo ya Service Excellence Awards (TSEA) 2025.

Taarifa ya Jubilee Health Insurance kwa vyombo vya habari imesema tuzo hiyo ambayo imetolewa Machi 28 mwaka huu inawafanya waongeze juhudi katika kutoa huduma bora kwa wateja, jambo ambalo limekuwa kipaumbele chao kila wakati.

Pia wanajivunia sana kupata tuzo hiyo ya heshima, ambayo inadhihirisha kazi ngumu ya timu yao na imani kubwa ambayo wateja wao wanayo kwao.

“Tuzo hii ni heshima kubwa kwetu,” amesema Veronica Nyage ambaye ni Mkuu wa Idara ya huduma kwa Wateja kutoka Jubilee Health Insurance.

“Tuzo hii inaonyesha jitihada na kujitolea kwa timu yetu yote, na tumejizatiti kuendelea kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu.”

Jubilee Health Insurance itaendelea kuzingatia kuridhika kwa wateja na ubora wa huduma, ikijivunia mafanikio haya na kuhakikisha huduma za afya bora zaidi kwa Watanzania.

"Asante kwa wateja wetu, washirika, na wafanyakazi wetu kwa msaada wao usio na kikomo. Tunatarajia kufikia mafanikio makubwa zaidi pamoja."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...