Na Diana Byera, Missenyi
TIMU ya uratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia imetatua changamoto ya mtoto Lovenes miaka 13 anayeishi Kijiji cha Bubale ambaye hajawai kwenda shule na kufanishwa hitaji lake la kujiunga na elimu ya watu wazima katika shule ya Msingi ya Bubale wilayani Missenyi.
Mtoto Lovenes aliwafuata Waratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria na kuwapigia magoti na kuwa kama atafanikiwa kuanza elimu ya shule ya msingi na kupata elimu ya watu wazima akajua kusoma na kuandika atasimulia maisha yake yote kwamba kampeni hiyo iliwai kumuletea mafanikio makubwa maishani mwake.
"Simujui baba yangu na mama yangu yuko nchini Uganda,nimeishi maisha ya kuhama hama na nimekuwa mtumwa wa kazi za ndani ,mjomba wangu ameniokoa kutoka kwenye utumwa wa kazi za ndani ,matumaini yangu leo ni kuunganishwa na mwalimu ili niende shuleni.Kama nitaanza shule nikajua kusoma na kuandika basi itakuwa simulizi maisha yangu yote,”amesema.
Loveness alionekana mtoto peke yake kati ya mamia waliokusanyika kupata huduma za msaada wa kisheria lakini alisema kama timu inaweza kununua vifaa vya shule na akajua kusoma na Kuandika pamoja na kuamka kwenda shuleni kama watoto wengine basi hataweza kusahau jina linaloitwa Mama Samia.
Mtoto huyo amemwambia mratibu wa kampeni hiyo ya msaada wa kisheria wilayani Missenyi kuwa hajawai kumujua baba yake isipokuwa mama yake ambaye anakimbia mara nyingi na kumuacha pamoja na mjomba wake ambaye sasa amemuondoa sehemu za mateso alikokuwa ameajiliwa na mtu maeneo ya Kagera Suger.
"Sijui kuandika jina langu wala la baba yangu,sijui chochote moyoni mwangu nilifikiria kuwa kama wageni wanaokuja wanasikiliza changamotoo za watu wenye matatizo basi na mimi kama mtoto nitajipeleka niwasilishe tatizo langu la kipekee ili iwe mara yangu ya kwanza kusaidiwa kutimiza ndoto yangu ya kusoma na naomba mnisaidie niende Shuleni nikasome.”
Kwa upande wa Mratibu wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia wilayani Missenyi Maximilian Fransis baada ya kupokea kilio hicho aliwasiliana na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Rubale ambapo amesema yuko tayari kumpokea na kumusajili shuleni kwa mfumo wa Elimu ya watu wazima.
Mratibu huyo pamoja na wajumbe wa kamati wamemhakikisha mtoto huyo atapata mahitaji yote shule ambapo amenunuliwa madafutari ,sare za shule,pesa ya viatu,na sweta ili kuanza safari yake ya kusoma.
Wakati huo huo Mjomba wa mtoto huyo Enias amesema yeye anazaliwa na dada zake wawili dada yake mmoja amepotelea nchini Uganda na mwingine amefariki, hivyo baada ya kupata taaarifa kuwa wanawatoto alianza kutafuta namna ya kuwa weka pamoja na kuwatoa kwenye mateso.
Amesema kampeni hiyo itafanya hata watoto waliokwama na waliositishwa masomo kurudi shuleni ili watimize ndoto zao huku akihaidi kuwalea watoto wa dada zake kama mzazi na kuwasahahulisha manyanyaso ambayo wamekuwa wakiyapitia huko nyuma.
Ametoa shukurani kwa serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuibua changamoto na kuwafata wananchi katika vijiji vya pembezoni ,kwani wanachangamoto nyingi za kisheria na hawana gharama za kuwalipa mawakili ili kushinda kesi zao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...